Wednesday, 5 February 2014
Saturday, 1 February 2014

Nabii Flora
SALAMU ZA NABII FLORA
Ninawasalimu kwa jina la Yesu, ninawakaribisha katika kipindi kizuri cha neno na uzima, uponyaji na miujiza, wakati huu ni kipindi cha neno. Kabla sijaongea chochote nitaongea na Mungu kwaajili ya kumaliza mwezi huu mwezi Abuu, ambao anamwambia Nabii Ezekieli kwamba waambie watu wangu wana wa Israeli huu ni mwezi kwao wa Baraka, utakuwa ni mwezi kwao wa majibu.

KUOMBEA VIJANA AJIRA
Kabla sijaomba nimeambiwa na Mungu usiku wa leo kipindi
tunamaliza mwezi nimeona kunavijana wanatamani ajira lakini hawana ajira. Baba
wabariki vija kabla hatujamaliza mwezi, ulisema utaruhusu wingi wa Baraka za
pesa, ajira, utajiri 1, 2, 3 vijana wote pokea.

Baba nahitaji vijana hawa wakusujudie maana umesema wakuabuduo watakuabudu katika Roho na kweli,
Baba nahitaji watu hawa uwabariki Mungu, nafungua kamba mikononi mwenu, kuna
watu wamekamata pesa azikai mpo hapa nataka leo mumsujudie huyu Mungu
aliyetamalaki katika matuo haya wote sujudu pokea. Kwa Damu ya Yesu Kristo
ulisema kila goti litapigwa asema Bwana na kila ulimi utakiri, sujudu mbele za
Bwana Mungu wa majeshi.

KIPINDI CHA MAOMBEZI
NA UPONYAJI
Hawa ni watumishi wa Mungu tena aliye hai, tunamtangaza
Mungu aliye hai, kwa neno la ufunuo ishara na miujiza iliwatupeleke mbinguni
kwa yeye aliye hai. Nipo hapa kwaajili ya kusogeza kupeleka juu ya meza kuu
kwake yeye aliye hai, lazima tumjue Mungu wa kweli ndipo tuweze kufanikiwa.
Lazima tumjue Mungu anayetenda, watumishi wakipakwa mafuta wanapaswa
kuheshimiwa.

Nasema na watu pokea nakufungua vifungo vyako, umekaa mwezi
mzima ujapata pesa toka mwaka umeingia leo ni miezi mitano hujafanikiwa leo ni
siku yako ya kufanikiwa, pokea baraka nasema pokea. Nazungumza na watu
mnaoniangalia, wageni mbalimbali nasema pokea wafanya biashara nasema na ninyi
leo.

Nasema kuna watu wamefungwa vifungo kichwani wanasikia sauti
za ajabu, umekuwa ukisikia sauti inakwambia utakufa, nakutamkia haufi. Pokea baraka
sasa, kuna watu wenye Kansa, Ukimwi leo uponyaji unaingia, pokea kupona wewe mwenye pepo la Ukimwi pepo la Kansa
nakufuatili kwa moto mkali nakukausha achilia watu sasa, oooh Yesu nakuita
nakuita Baaba leo ninakausha Ukimwi watu elfu moja mia tano wanakwenda kupima
watakuta negative.

Kuna watu wanamajini mahaba yamekufunga hupati kazi, huolewi
nasema inuka umekuwa ukifanya mapenzi na
mtu usiyemjua, yapo majini mahaba yanatoka wengine virusi vya Ukimwi leo
vinatoka. Yesu anatembea lazima atembee kwako leo tunakwenda kuingia mwezi mpya,
nakwambia ruka kamba zako zinakwenda kukatika leo pokea nafasi ya kuwa
mkurugenzi lazima upate.

Lazima tugawe mwaka na baraka zetu hujaolewa utakwenda
kuolewa, hujapata mtoto hutapata mtoto, hujapokea ujauzito utapokea, nasema na
watu wenye masikio. Ninakuapia kw ajina la Yesu mwanao atasoma shule kama kulikuwa
na mtu anamloga hata mloga tena, nasema nikiwa na uhakika na Mungu ninaye
mtumikia, Mungu wangu ni Mungu anayeona.

Lazima tuvuke mwezi wa sita na vitu vyetu, waume zetu, wake,
watoto, ng’ombe lazima tuvuke na baraka na upako wetu. Baba zibitisha neno hili
kwa ishara watu hawa sikia manukato hapa, naigeuza hewa ya mahali hapa na pia
watu hawa wapigwe tiki wengine waone baraka mikononi mwao. Na pia hewa geuka
unayenisikia hewa ya mahali hapa nakugeuza ugeuke kuwa baraka, watu wavutapo
hewa hii wapokee mafanikio naseama hewa geuka kuwa manukato mazuri na kuwa
baridi na kuwa mafanikio, naamuru mafanikio madhabahu toa moto nasema hewa
geuka.


Hii ni huduma ya maombezi maana yake manukato, katika Ufunuo
5:8, nasema Bwana tembea katika huduma hii ya manukato naigeuza hewa nasema
hewa geuka watu wapokee manukato, watasikia manukato mazuri ooh Yesu tembea na kuwa manukato mazuri. Hata
mtumishi wa Mungu Rulea Sanga apokee Baraka juu ya kazi zake Yesu akuinue pokea
manukato mazuri.


Oooh Baba tembea umetukuka
Jehova umetukuka naigeuza hewa, maana ya manukato ni maombi yetu yamepewa
kibali mbele za Mungu, wagonjwa wa Ukimwi wameponywa, mkansa zimeponywa, maana
ya manukato utasoma katika Ufunuo. Andiko limeandika katka Ufunuo nikaona
chetezo moshi ukatanda wa arufu nzuri hayo ni maombi ya watakatifu.
Ufunuo 8:3
Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo
cha dhahabu akapewa uvumba mwingi iliautie pamoja na maombi ya watakatifu juu
ya madhabahu ya dhahbu iliyo mbele ya kiti cha enzi. Malaika mwingine akaja
akasimama mbele ya madhabahu mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi
iliautie pamoja na maombi ya watakatifu juu ya madhabahu ya dhahabu iliyombele
ya kiti cha enzi. Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na
maombi ya watakatifu.
Sikumoja niliona moshi unapanada chumbani kwangu unakwenda
juu nikasikia sauti inaniambia maombi yako yamekubalika mbele za Bwana,
yamekuwa manukato mbele za Mungu. Kumbe ule moshi ukipanda juu ni manukato
mbele za Mungu, ukiona unaomba tu moshi unatokea jua anayekuongoza amekubaliwa
na Mungu.
UJUMBE WA LEO UTATOKA
KATIKA KITABU CHA YOELI
Yoeli 2:21-27
Ee nchi usiogope furahi na kushangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo
makuu, msiogope enyi wanyama wa kondeni maana malisho ya jangwani yanatoa miche
; anasema ee nchi shangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu tangu
mwezi wa kwanza hadi huu wa tano. Hata kama uchumi wako ulikuwa umekauka,
nyumbani kwako kulikuwa na jangwa katika mwezi huu Abuu lazima mimea yako
itatoa miche, palipo kuwa na jangwa patatoa maji, ulikuwa imesimamishwa kazi
utarudishwa kazini, ulikuwa huapata promotion utapata, anasema enyi nchi furahi
sana na kushangilia kwa kuwa tazama mimea inatoa miche palipo na jangwa lakini
hasubuhi ya leo patakuwa na baraka.
Hata kama ulikuwa na ukame
wa fedha Bwana ataruhusu baraka za pesa zitakuja kwako, nasema pokea kabla hatujavuka
mwezi. Yesu atafanya kitu kwako zipo siku nne mbele akaunti zako utazikuta
zimejaa, ikiwayule baba muhaya amepata laki saba wiki hii iweje wewe usipae,
anasema nchi usiogope ujapotishwa ukaambiwa
utasimamishwa kazi usiogope nchi tazama malisho ya kondeni yanatoa miche
hata nyie wanyama wa kondeni msiogope maana palipo na jangwa patatoa maji siku
ya leo.
Na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu unatoa nguvu zake; maana
ya mti ni mtu yaani wewe mwanadamu uliyefika mahali hapa utazaa matunda yake,
utakuwa kama mti uliopandwa katika vijito vya maji tena uzaao matunda kwa
majira yake. Nakutamkia kufanikiwa, nakutamkia kuwa kama mti ulipandwa katika
vijito vya maji unakwenda kuvuka mwezi mwingine, nataka Mungu akutendee wewe,
lazimaMungu aruhusu baraka kwako zitoke za kila aina.
Ujapo kaa miezi mi tano hujafanikiwa usiogope ewe Mtanzania,
furahia na kushangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu leo. Lazima Bwana
atatenda kwako mambo makuu, pakiwa na ukame pataamuriwa maji kutoka anasema na
mti utatoa matunda yake yaani familia yako inakwenda kutoa baraka za kila aina
leo, nakupa ufunguo wa baraka hujaolewa nakupa funguo ya kuolewa, hujaendesha
gari nakupa funguo ya gari, hujapata mtoto nakukabidhi funguo wa mtoto pokea
sasa furahi na kushangilia.
Yaani tarajia kabisa leo hii ukitoka hapa maisha yako
yatakwenda kufunguliwa. Nakuapia kwa jina la Yesu lile jiwe litabiringishwa
asema Bwana wa majeshi, lazima huinuke, hufanikiwe kiuchumi lazima maisha yako
yabadilike. Uliyefika hapa umetumia nauli Yesu azihesabu hatua zako akubariki
wewe uliyefika hapa lazima Yesu atende mambo makuu.kumbe katika mzabibu pia
kunanguvu, ndio maana watu tunawapa mzabibu. Yesu alisema yeye ni mzabibu wa
kweli anywae mzabibu na kuinywa Damu
yake ataona mauti naye atafanikiwa na kustawi sana .
Na kwambia haijalishi watu wamefunga mambo yako, ulikuwa unapafomu vizuri shuleni
sasa virus amekula nakutamkia ukitoka hapa mambo yako yatakuwa safi. Usiogope
nchi furahi na kushangilia kwa kuwa Bwana
ametenda mamboa makuu. Haijalishi umefungwa tumbo lako toka mwezi wa
kwanza hadi mwezi wa tano hujajibiwa, nakwambia mti huu utatoa nguvu zake na
mzabibu huu utatoa nguvu zake.
Lazima watu wafunguliwe leo, ninaona vijana wanaangaika
hawana ajira, watu wanakula chakula cha shida na kulala kwa shida leo
nakutamkia hadui zako waliweka ukuta nitauporomosha lazima uvuke, nikutoe
ng’ambo nikuvushe katika mto Neriba.
Furahini basi enyi wana wa Sayuni mkamfurahiye Bwana Mungu wenu; watu
wamepona vipofu wameona, watu wamepona Ukimwi anasema enyi wana wa Sayuni
furahini basi, napenda kuona watu wakifurahi asubuhi ya leo ebupokea baraka za
kufurhi sasa, anasema furahini na kushangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo
makuu.
Kwa kuwa ninyi huwapa mvua tena kipimo cha haki, huwapa ninyi mvua ya
masika kwa kipimo cha haki, Naye uwanyeshea
mvua, mvua ya masika na mvua ya vuli; nataka Bwana akupe kipimo cha
haki Yesu akupe baraka usibaki chini kijana Yesu akupe kipimo cha haki. Maana
ya mvua ni Baraka, anaseama atawanyeshea mvua kama kwanza yaani ataziruhusu
baraka kama hapo kwanza, kama ulikuwa na maduka ukafilisika tarajia kuibuka,
ulikuwa na cheo kikubwa tarajia kupandishwa, ilikuwa milango imefungwa tarajia
kupata pesa pokeaaaa! kwa jina la Yesu.
Naachilia fataki watu waponywe leo, watu wamefurahiya na
kushangilia kwa kuwa Mungu ametenda mambo makuu, hupo hapa mama umefungwa na
wachawi hupati mtoto nalifungua tumbo lako pokea funguka leo, majini mahaba yanaondoka,
mchumba aliyekuacha anakurudia, mume wako anarudi, nafasi ya kazi inarudi
mshahara unaongezewa.
Yamkini wewe umekuwa hupati mafanikio, unasikia sauti
kichwani mwako inakwambia ondoka hapa acha kazi hilo nipepo leo nalitoa 1, 2, 3
tooouuuuchhhh! Pokea funguka watu , nasema na watu leo. Kuna watu hapa mambo
yao hayaendi biashara zimeyumba ,
wengine wana presha, kisukari, Ukimwi, wengine wamefukuzwakazi, wengine hawana
mitaji, wengine Mungu wamezarauliwa bila sababu leo Bwana anasema furahi na
kushangilia kwa kuwa Yesu anatenda mambo makuu.
Unawatoto wako shuleni hawafanikiwi wakisoma wanafeli,
nakwenda kuangusha achia watu hawa 1, 2, 3 pokea kwa jina la Yesu naachilia mlipuko. Nasema lipo
pep[o ndani mwako leo naling’oa inuka jinni mahaba tooka achia watu
wanafunguliwa leo. Mme wako alikuwa
alali nyumbani leo atalala nyumbani, hupati pesa leo utapata pesa, hauna mtaji
pokea mtaji.
Na sakafu za kupeetea zitajaa zitajaa ngano na mashinikizo yatafurika
kwa divai na mafuta; mama unavyombo vyoko, masinia Bwana anakwenda
kujaza baraka, nyumba yako itajaa baraka sasa tunavuka na utajiri wetu. Nataka
tunapoingia mwezi wa sita tunatoka na baraka zetu watu wakajae kiuchumi, kifedha pokea sasa
kumiliki Baraka.
Baba watu hawa wapo tayari asubuhi ya leo kujazwa hazina zao,
mashinikizo yao wameinua mikono wanahitaji Mungu ujaze akaunti zao, ujaze kazi
zao, ujaze nyumba zao baraka. Nasema na watu wanao nitazama kwenye yuotube,
wanaonisoma kwenye blogu na facebook na waliofika hapa matuo haya kwamba wiki
ijapo itakuwa ni mwezi mpya nitakwambia mwezi unasimamia nini.
Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige na hata ile iliyoliwa
na parare na ile iliyoliwa na madumadu na maturutu ; yamkii baba au
mama, kijana upo hapa lakini kuna miaka yako iameliwa na nzige umefanya
biashara ulikuwa na maduka kariakoo, ulikuwa na maduka mwenge ya vinyago
ulikuwa na wateja wazungu leo wamekukimbia wote sasa nakurudishia wale wateja
wa vinyago wazungu kutoka Marekani. Nakurudishia leo ile miaka yako iliyoliwa
na nzige pokea sasa wateja.
Yamkini mama ulikuwa na miaka ya mafanikio, mlikuwa mkipanga
mipango mkiwa hanimoni kitandani vizuru mnaelewana lakini madumadu kala mwaka
wenu, maturutu kashambulia ndoa yenu sasa hivi mnalala mvungu wan ne mwanaume
amevaa jinsi sita mwanamke night dres saba, leo Bwana anakwenda kurejesha amani,
anakwenda kurejesha miaka yenu katika vitanda vyenu.
Nanyi mtakula chakula chenu na kushiba; anasema Bwana nasi
tutakula chakula tele tena na kushiba, Bwana anakwenda kutupa kushiba wewe
ambaye unakula robo kilo kwa sababu ya bajeti pesa zimeyumba Bwana anafungua
milango ya pesa leo naifungua sasa kwako, nasema pokea milango ya pesa
naifungua sasa utakula na kushiba Yesu atajaza.
Na kuliimidi jina la Bwana Mungu wenu aliye watendea mambo makuu; nataka
watu waliimidi jina la Bwana, kama hupo hapa kunamchawi alikuloga alikuendea
Bagamoyo, Kigoma mwishop wa reli, ameenda Sumba wanga, Nigeria amekuloga
nakwambia hapa imesimili kabisa hapa ngoma imedunda mwambie amechemka. Yule
Nabii akasema kwa kinywa cha Bwana kwamba popote walipokuwa wametufunga
tumekwisha kufunguliwa.
Nanyi mtajua mimi ni katikati ya Israeli na yakuwa mimi ndimi Bwana
Mungu wenu, wala hakuna Mungu mwingine na watu wangu hawata tahayari kamwe; haijalishi
chochote umenenewa wamesema mwanao hata soma ninakutamkia mwanao lazima asome,
hata kama mchawi atakuwa dirishani kwako lazima atainamishwa anashushwa kama
mpira asema Bwana wa majeshi lazima wewe ufanikiwe.
KUOMBEA VITAMBAA
Petro mtume aliponya wagonjwa kupitia vitambaa, nataka
mikono yako kila utakapogusa kitambaa upate mafanikio, palipo na giza patakuwa
na nuru, tunaingia mwezi wa sita mwezi
ambao nitakupa jina lake unaitwa Eluli yaani mwezi wa kutokewa. Kama
hujawahi kutokewa na malaika utatokewa mwezi wasita, hujawahi kusikia sauti ya
Mungu utaisikia. Nataka ukamate kitambaa cheupe kuashiria nyumba yako kama
kulikuwa kunagiza linakwenda kutoka. Baba tazama tendo hili la utukufu la
kusisimua na la kushangaza, maajabu na miujiza ambalo Baba Mungu mbingu
zimeikubali, Mungu umekubali kutoka mbinguni mtume Petro na Yohana waliponya
watu kupitia leso zao na mimi Baba nimewamilikisha vipawa, nimewapa vitambaa
vyeupe kinaashiria utukufu wa Mungu. Maana ya kitambaa cheupe ni utukufu,
ukamwingie kila mmoja utukufu palipokuwa na giza giza liondoke, maana Mungu
amesema tazama nuru yang’ara gizani na giza halikunishinda . nami ninasema
kupitia vitambaa hivi mambo yako yote yanakwenda kufunguka, palipo kuwa pagumu
patafanywa kuwa pepesi.
Nuru ikuangazie Pasta Ansila, Watumishi wa Mungu, Yesu
akafungue mbingu nasema kitambaa hiki kitakuwa Baraka ndani ya maisha yako
asubuhi shika na jioni hadi siku 21 utaona mambo yako yanafunguka. Wasio
kusalimia watakusalimia, utakanyaga sehemu isiyo kanyagika napo utapata kibali
natamka baraka sasa ninaachilia na tunaondoka na Baraka zetu za mwezi wa kwanza,
wa pili, wa tatu, wan ne, wa tano tunavuka nazo mto Yordani. Kwani miaka yetu
iliyoliwa na nzige tumerejeshewa, muzuri wetu umerejeshwa, maisha yetu marefu
yamerejeshwa, tumerejeshewa utajiri, watoto, vibali makazini, vyeo, afya zetu
CD4 zilizoshuka wapendwa zimerejeshwa kwa Damu ya Yesu.
SHUKRANI
Baba tumejionea kwa macho yetu na tumesikia kwa masiko yetu, nasi Baba sifa na utukufu tunakurudishia wewe, na tunakuomba Mungu wetu endelea kumtumia mtumishi wako Nabii Flora kuwatendea wengine ambao hawaja shuhudia ili Mungu waweze kushuhudia kile ulicho watendea katika jina la Yesu ninaomba na kushukuru Amen.
Tembelea:
MZEE WA UPAKO AVAMIWA
Mzee wa Upako

Haruni Sanchawa na Gladness Mallya
MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi – Utashinda, Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako usiku wa kuamkia jana alivamiwa kanisani na kundi la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kumteka kwa muda kabla ya kumpora mamilioni ya shilingi.
Gazeti hili lilifika eneo la tukio kanisani kwake, maeneo ya Ubungo Kibangu na kufanikiwa kupewa taarifa ya jinsi ujambazi huo ulivyofanyika ambapo mtoa habari alisema kundi la majambazi lilivamia kanisa hilo usiku.
“Kundi hilo la watu lilifika maeneo hayo majira ya saa tisa na kuwateka walinzi ambao walikuwepo hapo hadi saa kumi na moja alfajiri kuamkia jana,” alisema mtoa habari wetu kwa sharti la kutoandika jina lake gazetini.
Imedaiwa kuwa kabla ya kufanya uvamizi huo, mlinzi wa kanisa hilo (jina tulihifadhi kwa sababu za kiusalama ), alivamiwa na kufungwa kamba na baadaye kunyang’anywa bunduki na majambazi hao.
Chanzo chetu hicho cha habari kiliongeza kuwa baada ya kumkamata mlinzi huyo, majambazi hao walienda moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Lusekelo na kumteka kwa muda kabla ya kumuamuru atoe pesa alizokuwanazo vinginevyo wangemuua.
Habari zinasema Mzee wa Upako aliamua kutoa pesa ambazo inadaiwa ni zaidi ya shilingi milioni 20 ambazo inaaminika zilitokana na sadaka za waumini wake. Kiongozi huyo wa kanisa hakujeruhiwa.
Habari za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa Mchungaji Lusekelo hakai kanisani hapo na kwamba ni mara chache hulala katika nyumba hiyo ya ibada hasa anapokuwa na kazi maalum.
Gazeti hili lilipowasiliana na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga alikiri kutokea kwa tukio hilo na amedai kuwa hadi sasa watu wawili wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.
“Uzoefu unaonyesha kuwa kuna baadhi ya makampuni ya ulinzi hapa nchini yana watumishi ambao si waaminifu, natoa wito kwa wamiliki wa makampuni binafsi ya ulinzi kabla ya kuajiri mlinzi , yahakikishe uaminifu wake kwanza,” alisema Kalinga.
Aliongeza kuwa kampuni za ulinzi zinalinda mamilioni ya mali za watu lakini anashangazwa kuona baadhi ya walinzi wao wanauza siri za muajiri wao kwa watu wasio raia wema.
Waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta Mzee wa Upako ili kusikia kauli yake juu ya tukio hilo bila mafanikio.
Kwa mujibu wa walinzi waliokutwa kanisani hapo ambao hawakupenda majina yao kuandikwa gazetini, kiongozi huyo alikuwa amekwenda nyumbani kwake Mbezi kupumzika.
Source:wokovuimelda.blogspot.com/
Saturday, 25 January 2014
AVID ROBERT ANAYETARAJIA KUFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA MUZIKI WA INJILI TANZANIA
“ Miaka ya nyuma muziki wa injili ulidharaulika sana na mtu alipoonekana akiimba muziki huo alionekana kama kituko fulani hivi kwa sababu hakuna aliyekuwa anaguswa na nyimbo hizo.
Sio kwamba kipindi hicho hapakuwa na waimbaji wazuri wa muziki huo, la hasha! Walikuwepo tena wakali pengine kuliko waimbaji wa leo wanao mwimbia Mungu nyimbo za injili. Miaka hiyo kulikuwa na waimbaji kama Epharaem Mwansasu, Faustini Munishi, Mungu Four, Ency Mwalukasa, Jenifa Mgendi na miaka ya hivi karibuni alijitokeza Cosmas Chidumule aliyekuwa anapiga muziki wa dunia.
Na miaka hiyo ilikuwa ni mara moja sana kusikia muziki wa injili kukipingwa katika kumbi za starehe kama bar, kwenye harus nk. Lakini leo hii upepo umebadilika,”. Ndivyo alivyoanza kusema nami mwanamuziki mahiri wa muziki wa injili nchini David Robert aliyeibuka katika anga la muziki huo mwaka 2002 na albamu ya Baba.
Katika albamu hiyo Robert ambaye ana sauti nzito alishilikiana vema na Godwin Gondwe ambaye naye anasauti ya zege na kuifanya albamu hiyo kuwa na muvuto wa pekee na kuweka imara katika anga la muziki huo.
Albamu hiyo iliyokuwa ni nyimbo kumi iliwashika wengi na kila mmoja kupenda kuzisikiliza. Nyimbo zilikokuwa katika albamu hiyo ni Baba, Niongoze, Ngulujangu (kinyakyusa), Nakupenda, Hosana, Tufani, Mimi nani?, Bwana atafanya njia na We njoo.
Kufanya vizuri sokoni kwa albamu hiyo kulikuwa kama kumemtoa tongotongo machoni Robert. Kwani mwaka 2003 alilazimika tena kuingia studio na kufyatua albamu ya pili inayojulikana kwa jina la Kiganjani pa Mungu.
Albamu hiyo nayo imewakamata vema wapenzi wa muziki huo na kuanza kumtaka arekodi mkanda wa video ili iwe rahisi kwao kuwa wanamuona kwa njia hiyo japo wako naye mbali.
Albamu ya Kiganjani pa Mungu ilikuwa na nyimbo 8 ambao ni Neema, Sema nami, Shukurani, Nitakumbuka, E Yesu, Yesu ni Mungu na Kiganjani pa Mungu unaobeba albamu.
Hakuna asiyeelewa kila kitu kinachotengezwa kwa ubora, hutumia gharama kubwa kukikamilisha. Mwimbaji huyo alilitambua hilo baada ya kuona wapenzi wa muziki wake kumtaka arekodi hizo katika mtindo wa video.
Hata hivyo Robert alikaa na kutafari, kwa makini jinsi gani anaweza kurekodi video ambayo inaweza kuwa tofauti na video zilizotangulia. Jibu lake lilionekana kuwa ni kujiweka sawa katika fungu la fedha.
Robert aliamua kuzichambua nyimbo zilizo katika albamu hizo mbili na kufanikiwa kurekodi albau moja aliyoipa jina la The Best Of David Robert ambayo tayari iko sokoni kuanzia wiki iliyopita na inapatikana kwa njia ya HVS, DVD, na VCD.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa albamu hiyo imerokodiwa katika madhari nzuri na mtaalam wa masuala ya filamu kutoka nchini Ujerumani Daniel Uphaus kwa kushirikiana na Sye ambaye ni mtaalamu wa kuongoza filamu.
Wataalu hao wameirekodi kwa makini albamu hiyo hali iliyopelekea kukubalika katika soko la kimataifa, ambapo tayari vituo vya Chanel O na Mtv Base wameiomba kwa ajili ya kuirusha katika runinga zao.
Ubora wa albamu hiyo ya The Best of David Robert umetokana na maandalizi ya miaka mitatu aliyoyafanya kabla ya kuchukua uamuzi wa kuingia studio na kutoa kitu hicho ambacho kinamvuto mkubwa.
Kukamilika kwa albamu hiyo kulichukua miezi minne na baada ya kurekodiwa aliipeleka kwa wataalam wengine kabla ya kuingia sokoni. Katika kuhakikisha albamu hiyo inakuwa tofauti na albamu nyingine hasa za muziki wa injili nchini, Robert alisafiri mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata picha nzuri kutokana na ujumbe wa nyimbo husika.
Mikoa aliyofanikiwa kwenda kurekodi albamu hiyo ni Morogoro, Iringa, Arusha, Moshi, Pwani na Dar es Salaam.
Aliyemvutia katika anga la muziki wa injili
Robert alisema kuwa huduma ya uimbaji alikuwa nayo tangu akiwa mtoto, ana alipokuwa shuleni huduma hiyo aliifanya kwa nguvu zote kwa kutembelea shule mbalimbali kwa lengo la kutoa injili ya njia ya nyimbo mwaka 1998 na kipindi hicho alikuwa akisoma shule ya sekondali Jitegemee ya jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kuipenda huduma hiyo, Mhungaji Elpham Mwansasu, Mchungaji Daniel Richard Mwansumbi na Cosmas Chidumule ndiyo waliompa hamasa kubwa Robert kujikita katika anga la muziki huo wa injili. Waimbaji hao ndio walikuwa wakimvutia kutokana na sauti zao kuwa nzuri pamoja na ujumbe wa nyimbo uliokuwemo ndani ya nyimbo hizo.
Mafanikio aliyoyapata kutoka na huduma ya uimbaji wa muziki huo
Kupitia muziki huo wa injili Robert amefaniki kujenga nyumba nzuri ya kisasa, ana gari nzuri. Mafaniko mengine alisema ni pamoja na kupata mtandao mzuri wa marafiki ndani na nje ya nchi na ana miradi mbalimbali inayomsaidia kuendesha maisha yake ya kila siku.
Matatizo anayokumbana nayo
Kuwa na mtaji mdogo wa kuitangaza huduma ya Mungu ndani na nje ya nchi, kutumia gharama kubwa katika kurekodi albamu na mwisho wa siku anajikuta mfukoni hana kitu.
Wito kwa wanamuziki wa injili hapa nchini
Anakerwa na waimbaji wanao kukimbilia katika muziki huyo kwa kuangalia pesa zaidi kuliko huduma. Ambapo watu wengi wamekuwa wakijikuta wanashindwa kufanya vema kazi ya Mungu pindi wanachokitarajia wanapokikosa.
Mwanamuziki anayemzimikia zaidi
Bila kificho David Robert alisema kuwa muimbaji mwenzake anayetamba na albamu ya Unikumbe Christina Shusho, ndiye anayemzimikia zaidi kutokana na nyimbo zake kuwa na ujumbe muzito ambao mara nyingi nyimbo hizo hugusa maisha anayopitia.
Matarajio yake ya baadaye
Ni kufanya mapinduzi makubwa katika muziki wa injili kwa siku za usoni. Mbali na hilo anatarajia kufanya uzinduzi wa albamu hiyo mwishoni mwa mwaka ujao. Je unamaoni gani kuhusu huduma ya David Robert? Usisite kunitumia maoni yako.
Subscribe to:
Posts (Atom)