Saturday, 1 February 2014




 Nabii Flora

SALAMU ZA NABII FLORA
Ninawasalimu kwa jina la Yesu, ninawakaribisha katika kipindi kizuri cha neno na uzima, uponyaji na miujiza, wakati huu ni kipindi cha neno. Kabla sijaongea chochote nitaongea na Mungu kwaajili ya kumaliza mwezi huu mwezi Abuu, ambao anamwambia Nabii Ezekieli kwamba waambie watu wangu wana wa Israeli huu ni mwezi kwao wa Baraka, utakuwa ni mwezi kwao wa majibu.



KUOMBEA VIJANA AJIRA
Kabla sijaomba nimeambiwa na Mungu usiku wa leo kipindi tunamaliza mwezi nimeona kunavijana wanatamani ajira lakini hawana ajira. Baba wabariki vija kabla hatujamaliza mwezi, ulisema utaruhusu wingi wa Baraka za pesa, ajira, utajiri 1, 2, 3 vijana wote pokea.
 
 
 Ee Mungu uliyetukuka ninakwenda kuachilia upako wa ajira kwa vijana hawa, upako wa pesa wameshindwa wengine kuoa kwa sababu ya fedha wengine maisha yao yameyumba, wanalala wanakuwa kama wamechanganyikiwa Baba maisha yamekuwa magumu leo naachilia wingu la Baraka, naziinamisha mbingu juu yenu 1, 2, 3 tooouuuchhhh


Baba nahitaji vijana hawa wakusujudie maana umesema  wakuabuduo watakuabudu katika Roho na kweli, Baba nahitaji watu hawa uwabariki Mungu, nafungua kamba mikononi mwenu, kuna watu wamekamata pesa azikai mpo hapa nataka leo mumsujudie huyu Mungu aliyetamalaki katika matuo haya wote sujudu pokea. Kwa Damu ya Yesu Kristo ulisema kila goti litapigwa asema Bwana na kila ulimi utakiri, sujudu mbele za Bwana Mungu wa majeshi.



KIPINDI CHA MAOMBEZI NA UPONYAJI
Hawa ni watumishi wa Mungu tena aliye hai, tunamtangaza Mungu aliye hai, kwa neno la ufunuo ishara na miujiza iliwatupeleke mbinguni kwa yeye aliye hai. Nipo hapa kwaajili ya kusogeza kupeleka juu ya meza kuu kwake yeye aliye hai, lazima tumjue Mungu wa kweli ndipo tuweze kufanikiwa. Lazima tumjue Mungu anayetenda, watumishi wakipakwa mafuta wanapaswa kuheshimiwa.
 

Nasema na watu pokea nakufungua vifungo vyako, umekaa mwezi mzima ujapata pesa toka mwaka umeingia leo ni miezi mitano hujafanikiwa leo ni siku yako ya kufanikiwa, pokea baraka nasema pokea. Nazungumza na watu mnaoniangalia, wageni mbalimbali nasema pokea wafanya biashara nasema na ninyi leo.



Nasema kuna watu wamefungwa vifungo kichwani wanasikia sauti za ajabu, umekuwa ukisikia sauti inakwambia utakufa, nakutamkia haufi. Pokea baraka sasa, kuna watu wenye Kansa, Ukimwi leo uponyaji unaingia, pokea kupona  wewe mwenye pepo la Ukimwi pepo la Kansa nakufuatili kwa moto mkali nakukausha achilia watu sasa, oooh Yesu nakuita nakuita Baaba leo ninakausha Ukimwi watu elfu moja mia tano wanakwenda kupima watakuta negative.


Kuna watu wanamajini mahaba yamekufunga hupati kazi, huolewi nasema inuka  umekuwa ukifanya mapenzi na mtu usiyemjua, yapo majini mahaba yanatoka wengine virusi vya Ukimwi leo vinatoka. Yesu anatembea lazima atembee kwako leo tunakwenda kuingia mwezi mpya, nakwambia ruka kamba zako zinakwenda kukatika leo pokea nafasi ya kuwa mkurugenzi lazima upate.



Lazima tugawe mwaka na baraka zetu hujaolewa utakwenda kuolewa, hujapata mtoto hutapata mtoto, hujapokea ujauzito utapokea, nasema na watu wenye masikio. Ninakuapia kw ajina la Yesu mwanao atasoma shule kama kulikuwa na mtu anamloga hata mloga tena, nasema nikiwa na uhakika na Mungu ninaye mtumikia, Mungu wangu ni Mungu anayeona.



Lazima tuvuke mwezi wa sita na vitu vyetu, waume zetu, wake, watoto, ng’ombe lazima tuvuke na baraka na upako wetu. Baba zibitisha neno hili kwa ishara watu hawa sikia manukato hapa, naigeuza hewa ya mahali hapa na pia watu hawa wapigwe tiki wengine waone baraka mikononi mwao. Na pia hewa geuka unayenisikia hewa ya mahali hapa nakugeuza ugeuke kuwa baraka, watu wavutapo hewa hii wapokee mafanikio naseama hewa geuka kuwa manukato mazuri na kuwa baridi na kuwa mafanikio, naamuru mafanikio madhabahu toa moto nasema hewa geuka.
Hii ni huduma ya maombezi maana yake manukato, katika Ufunuo 5:8, nasema Bwana tembea katika huduma hii ya manukato naigeuza hewa nasema hewa geuka watu wapokee manukato, watasikia manukato mazuri  ooh Yesu tembea na kuwa manukato mazuri. Hata mtumishi wa Mungu Rulea Sanga apokee Baraka juu ya kazi zake Yesu akuinue pokea manukato mazuri.
 Oooh Baba tembea umetukuka Jehova umetukuka naigeuza hewa, maana ya manukato ni maombi yetu yamepewa kibali mbele za Mungu, wagonjwa wa Ukimwi wameponywa, mkansa zimeponywa, maana ya manukato utasoma katika Ufunuo. Andiko limeandika katka Ufunuo nikaona chetezo moshi ukatanda wa arufu nzuri hayo ni maombi ya watakatifu.
 Ufunuo 8:3
Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu akapewa uvumba mwingi iliautie pamoja na maombi ya watakatifu juu ya madhabahu ya dhahbu iliyo mbele ya kiti cha enzi. Malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi iliautie pamoja na maombi ya watakatifu juu ya madhabahu ya dhahabu iliyombele ya kiti cha enzi. Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu.
Sikumoja niliona moshi unapanada chumbani kwangu unakwenda juu nikasikia sauti inaniambia maombi yako yamekubalika mbele za Bwana, yamekuwa manukato mbele za Mungu. Kumbe ule moshi ukipanda juu ni manukato mbele za Mungu, ukiona unaomba tu moshi unatokea jua anayekuongoza amekubaliwa na Mungu.
UJUMBE WA LEO UTATOKA KATIKA KITABU CHA YOELI
Yoeli 2:21-27
Ee nchi usiogope furahi na kushangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu, msiogope enyi wanyama wa kondeni maana malisho ya jangwani yanatoa miche ; anasema ee nchi shangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu tangu mwezi wa kwanza hadi huu wa tano. Hata kama uchumi wako ulikuwa umekauka, nyumbani kwako kulikuwa na jangwa katika mwezi huu Abuu lazima mimea yako itatoa miche, palipo kuwa na jangwa patatoa maji, ulikuwa imesimamishwa kazi utarudishwa kazini, ulikuwa huapata promotion utapata, anasema enyi nchi furahi sana na kushangilia kwa kuwa tazama mimea inatoa miche palipo na jangwa lakini hasubuhi ya leo patakuwa na baraka.
Hata kama ulikuwa na ukame  wa fedha Bwana ataruhusu baraka za pesa  zitakuja kwako, nasema pokea kabla hatujavuka mwezi. Yesu atafanya kitu kwako zipo siku nne mbele akaunti zako utazikuta zimejaa, ikiwayule baba muhaya amepata laki saba wiki hii iweje wewe usipae, anasema nchi usiogope ujapotishwa ukaambiwa  utasimamishwa kazi usiogope nchi tazama malisho ya kondeni yanatoa miche hata nyie wanyama wa kondeni msiogope maana palipo na jangwa patatoa maji siku ya leo.
Na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu unatoa nguvu zake; maana ya mti ni mtu yaani wewe mwanadamu uliyefika mahali hapa utazaa matunda yake, utakuwa kama mti uliopandwa katika vijito vya maji tena uzaao matunda kwa majira yake. Nakutamkia kufanikiwa, nakutamkia kuwa kama mti ulipandwa katika vijito vya maji unakwenda kuvuka mwezi mwingine, nataka Mungu akutendee wewe, lazimaMungu aruhusu baraka kwako zitoke za kila aina.
Ujapo kaa miezi mi tano hujafanikiwa usiogope ewe Mtanzania, furahia na kushangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu leo. Lazima Bwana atatenda kwako mambo makuu, pakiwa na ukame pataamuriwa maji kutoka anasema na mti utatoa matunda yake yaani familia yako inakwenda kutoa baraka za kila aina leo, nakupa ufunguo wa baraka hujaolewa nakupa funguo ya kuolewa, hujaendesha gari nakupa funguo ya gari, hujapata mtoto nakukabidhi funguo wa mtoto pokea sasa furahi na kushangilia.
Yaani tarajia kabisa leo hii ukitoka hapa maisha yako yatakwenda kufunguliwa. Nakuapia kwa jina la Yesu lile jiwe litabiringishwa asema Bwana wa majeshi, lazima huinuke, hufanikiwe kiuchumi lazima maisha yako yabadilike. Uliyefika hapa umetumia nauli Yesu azihesabu hatua zako akubariki wewe uliyefika hapa lazima Yesu atende mambo makuu.kumbe katika mzabibu pia kunanguvu, ndio maana watu tunawapa mzabibu. Yesu alisema yeye ni mzabibu wa kweli anywae mzabibu na kuinywa  Damu yake ataona mauti naye atafanikiwa na kustawi sana .
Na kwambia haijalishi watu wamefunga  mambo yako, ulikuwa unapafomu vizuri shuleni sasa virus amekula nakutamkia ukitoka hapa mambo yako yatakuwa safi. Usiogope nchi furahi na kushangilia kwa kuwa Bwana  ametenda mamboa makuu. Haijalishi umefungwa tumbo lako toka mwezi wa kwanza hadi mwezi wa tano hujajibiwa, nakwambia mti huu utatoa nguvu zake na mzabibu huu utatoa nguvu zake.
Lazima watu wafunguliwe leo, ninaona vijana wanaangaika hawana ajira, watu wanakula chakula cha shida na kulala kwa shida leo nakutamkia hadui zako waliweka ukuta nitauporomosha lazima uvuke, nikutoe ng’ambo nikuvushe katika mto Neriba.
Furahini basi enyi wana wa Sayuni  mkamfurahiye Bwana Mungu wenu; watu wamepona vipofu wameona, watu wamepona Ukimwi anasema enyi wana wa Sayuni furahini basi, napenda kuona watu wakifurahi asubuhi ya leo ebupokea baraka za kufurhi sasa, anasema furahini na kushangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu.
Kwa kuwa ninyi huwapa mvua tena kipimo cha haki, huwapa ninyi mvua ya masika kwa kipimo cha haki,  Naye uwanyeshea mvua, mvua ya masika na mvua ya vuli; nataka Bwana akupe kipimo cha haki Yesu akupe baraka usibaki chini kijana Yesu akupe kipimo cha haki. Maana ya mvua ni Baraka, anaseama atawanyeshea mvua kama kwanza yaani ataziruhusu baraka kama hapo kwanza, kama ulikuwa na maduka ukafilisika tarajia kuibuka, ulikuwa na cheo kikubwa tarajia kupandishwa, ilikuwa milango imefungwa tarajia kupata pesa pokeaaaa! kwa  jina la Yesu.
Naachilia fataki watu waponywe leo, watu wamefurahiya na kushangilia kwa kuwa Mungu ametenda mambo makuu, hupo hapa mama umefungwa na wachawi hupati mtoto nalifungua tumbo lako pokea  funguka leo, majini mahaba yanaondoka, mchumba aliyekuacha anakurudia, mume wako anarudi, nafasi ya kazi inarudi mshahara unaongezewa.
Yamkini wewe umekuwa hupati mafanikio, unasikia sauti kichwani mwako inakwambia ondoka hapa acha kazi hilo nipepo leo nalitoa 1, 2, 3 tooouuuuchhhh! Pokea funguka watu , nasema na watu leo. Kuna watu hapa mambo yao hayaendi  biashara zimeyumba , wengine wana presha, kisukari, Ukimwi, wengine wamefukuzwakazi, wengine hawana mitaji, wengine Mungu wamezarauliwa bila sababu leo Bwana anasema furahi na kushangilia kwa kuwa Yesu anatenda mambo makuu.
Unawatoto wako shuleni hawafanikiwi wakisoma wanafeli, nakwenda kuangusha achia watu hawa 1, 2, 3 pokea kwa  jina la Yesu naachilia mlipuko. Nasema lipo pep[o ndani mwako leo naling’oa inuka jinni mahaba tooka achia watu wanafunguliwa leo.  Mme wako alikuwa alali nyumbani leo atalala nyumbani, hupati pesa leo utapata pesa, hauna mtaji pokea mtaji.
Na sakafu za kupeetea zitajaa zitajaa ngano na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta; mama unavyombo vyoko, masinia Bwana anakwenda kujaza baraka, nyumba yako itajaa baraka sasa tunavuka na utajiri wetu. Nataka tunapoingia mwezi wa sita tunatoka na baraka zetu  watu wakajae kiuchumi, kifedha pokea sasa kumiliki Baraka.
Baba watu hawa wapo tayari asubuhi ya leo kujazwa hazina zao, mashinikizo yao wameinua mikono wanahitaji Mungu ujaze akaunti zao, ujaze kazi zao, ujaze nyumba zao baraka. Nasema na watu wanao nitazama kwenye yuotube, wanaonisoma kwenye blogu na facebook na waliofika hapa matuo haya kwamba wiki ijapo itakuwa ni mwezi mpya nitakwambia mwezi unasimamia nini.
Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige na hata ile iliyoliwa na parare na ile iliyoliwa na madumadu na maturutu ; yamkii baba au mama, kijana upo hapa lakini kuna miaka yako iameliwa na nzige umefanya biashara ulikuwa na maduka kariakoo, ulikuwa na maduka mwenge ya vinyago ulikuwa na wateja wazungu leo wamekukimbia wote sasa nakurudishia wale wateja wa vinyago wazungu kutoka Marekani. Nakurudishia leo ile miaka yako iliyoliwa na nzige pokea sasa wateja.
Yamkini mama ulikuwa na miaka ya mafanikio, mlikuwa mkipanga mipango mkiwa hanimoni kitandani vizuru mnaelewana lakini madumadu kala mwaka wenu, maturutu kashambulia ndoa yenu sasa hivi mnalala mvungu wan ne mwanaume amevaa jinsi sita mwanamke night dres saba, leo Bwana anakwenda kurejesha amani, anakwenda kurejesha miaka yenu katika vitanda vyenu.
Nanyi mtakula chakula chenu na kushiba; anasema Bwana nasi tutakula chakula tele tena na kushiba, Bwana anakwenda kutupa kushiba wewe ambaye unakula robo kilo kwa sababu ya bajeti pesa zimeyumba Bwana anafungua milango ya pesa leo naifungua sasa kwako, nasema pokea milango ya pesa naifungua sasa utakula na kushiba Yesu atajaza.
Na kuliimidi jina la Bwana Mungu wenu aliye watendea mambo makuu; nataka watu waliimidi jina la Bwana, kama hupo hapa kunamchawi alikuloga alikuendea Bagamoyo, Kigoma mwishop wa reli, ameenda Sumba wanga, Nigeria amekuloga nakwambia hapa imesimili kabisa hapa ngoma imedunda mwambie amechemka. Yule Nabii akasema kwa kinywa cha Bwana kwamba popote walipokuwa wametufunga tumekwisha kufunguliwa.
Nanyi mtajua mimi ni katikati ya Israeli na yakuwa mimi ndimi Bwana Mungu wenu, wala hakuna Mungu mwingine na watu wangu hawata tahayari kamwe; haijalishi chochote umenenewa wamesema mwanao hata soma ninakutamkia mwanao lazima asome, hata kama mchawi atakuwa dirishani kwako lazima atainamishwa anashushwa kama mpira asema Bwana wa majeshi lazima wewe ufanikiwe.
KUOMBEA VITAMBAA
Petro mtume aliponya wagonjwa kupitia vitambaa, nataka mikono yako kila utakapogusa kitambaa upate mafanikio, palipo na giza patakuwa na nuru, tunaingia mwezi wa sita mwezi  ambao nitakupa jina lake unaitwa Eluli yaani mwezi wa kutokewa. Kama hujawahi kutokewa na malaika utatokewa mwezi wasita, hujawahi kusikia sauti ya Mungu utaisikia. Nataka ukamate kitambaa cheupe kuashiria nyumba yako kama kulikuwa kunagiza linakwenda kutoka. Baba tazama tendo hili la utukufu la kusisimua na la kushangaza, maajabu na miujiza ambalo Baba Mungu mbingu zimeikubali, Mungu umekubali kutoka mbinguni mtume Petro na Yohana waliponya watu kupitia leso zao na mimi Baba nimewamilikisha vipawa, nimewapa vitambaa vyeupe kinaashiria utukufu wa Mungu. Maana ya kitambaa cheupe ni utukufu, ukamwingie kila mmoja utukufu palipokuwa na giza giza liondoke, maana Mungu amesema tazama nuru yang’ara gizani na giza halikunishinda . nami ninasema kupitia vitambaa hivi mambo yako yote yanakwenda kufunguka, palipo kuwa pagumu patafanywa kuwa pepesi.
Nuru ikuangazie Pasta Ansila, Watumishi wa Mungu, Yesu akafungue mbingu nasema kitambaa hiki kitakuwa Baraka ndani ya maisha yako asubuhi shika na jioni hadi siku 21 utaona mambo yako yanafunguka. Wasio kusalimia watakusalimia, utakanyaga sehemu isiyo kanyagika napo utapata kibali natamka baraka sasa ninaachilia na tunaondoka na Baraka zetu za mwezi wa kwanza, wa pili, wa tatu, wan ne, wa tano tunavuka nazo mto Yordani. Kwani miaka yetu iliyoliwa na nzige tumerejeshewa, muzuri wetu umerejeshwa, maisha yetu marefu yamerejeshwa, tumerejeshewa utajiri, watoto, vibali makazini, vyeo, afya zetu CD4 zilizoshuka wapendwa zimerejeshwa kwa Damu ya Yesu.

SHUKRANI
Baba tumejionea kwa macho yetu na tumesikia kwa masiko yetu, nasi Baba sifa na utukufu tunakurudishia wewe, na tunakuomba Mungu wetu endelea kumtumia mtumishi wako Nabii Flora kuwatendea wengine ambao hawaja shuhudia ili Mungu waweze kushuhudia kile ulicho watendea katika jina la Yesu ninaomba na kushukuru Amen.
Tembelea: 

No comments:

Post a Comment