Saturday, 25 January 2014
AVID ROBERT ANAYETARAJIA KUFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA MUZIKI WA INJILI TANZANIA
“ Miaka ya nyuma muziki wa injili ulidharaulika sana na mtu alipoonekana akiimba muziki huo alionekana kama kituko fulani hivi kwa sababu hakuna aliyekuwa anaguswa na nyimbo hizo.
Sio kwamba kipindi hicho hapakuwa na waimbaji wazuri wa muziki huo, la hasha! Walikuwepo tena wakali pengine kuliko waimbaji wa leo wanao mwimbia Mungu nyimbo za injili. Miaka hiyo kulikuwa na waimbaji kama Epharaem Mwansasu, Faustini Munishi, Mungu Four, Ency Mwalukasa, Jenifa Mgendi na miaka ya hivi karibuni alijitokeza Cosmas Chidumule aliyekuwa anapiga muziki wa dunia.
Na miaka hiyo ilikuwa ni mara moja sana kusikia muziki wa injili kukipingwa katika kumbi za starehe kama bar, kwenye harus nk. Lakini leo hii upepo umebadilika,”. Ndivyo alivyoanza kusema nami mwanamuziki mahiri wa muziki wa injili nchini David Robert aliyeibuka katika anga la muziki huo mwaka 2002 na albamu ya Baba.
Katika albamu hiyo Robert ambaye ana sauti nzito alishilikiana vema na Godwin Gondwe ambaye naye anasauti ya zege na kuifanya albamu hiyo kuwa na muvuto wa pekee na kuweka imara katika anga la muziki huo.
Albamu hiyo iliyokuwa ni nyimbo kumi iliwashika wengi na kila mmoja kupenda kuzisikiliza. Nyimbo zilikokuwa katika albamu hiyo ni Baba, Niongoze, Ngulujangu (kinyakyusa), Nakupenda, Hosana, Tufani, Mimi nani?, Bwana atafanya njia na We njoo.
Kufanya vizuri sokoni kwa albamu hiyo kulikuwa kama kumemtoa tongotongo machoni Robert. Kwani mwaka 2003 alilazimika tena kuingia studio na kufyatua albamu ya pili inayojulikana kwa jina la Kiganjani pa Mungu.
Albamu hiyo nayo imewakamata vema wapenzi wa muziki huo na kuanza kumtaka arekodi mkanda wa video ili iwe rahisi kwao kuwa wanamuona kwa njia hiyo japo wako naye mbali.
Albamu ya Kiganjani pa Mungu ilikuwa na nyimbo 8 ambao ni Neema, Sema nami, Shukurani, Nitakumbuka, E Yesu, Yesu ni Mungu na Kiganjani pa Mungu unaobeba albamu.
Hakuna asiyeelewa kila kitu kinachotengezwa kwa ubora, hutumia gharama kubwa kukikamilisha. Mwimbaji huyo alilitambua hilo baada ya kuona wapenzi wa muziki wake kumtaka arekodi hizo katika mtindo wa video.
Hata hivyo Robert alikaa na kutafari, kwa makini jinsi gani anaweza kurekodi video ambayo inaweza kuwa tofauti na video zilizotangulia. Jibu lake lilionekana kuwa ni kujiweka sawa katika fungu la fedha.
Robert aliamua kuzichambua nyimbo zilizo katika albamu hizo mbili na kufanikiwa kurekodi albau moja aliyoipa jina la The Best Of David Robert ambayo tayari iko sokoni kuanzia wiki iliyopita na inapatikana kwa njia ya HVS, DVD, na VCD.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa albamu hiyo imerokodiwa katika madhari nzuri na mtaalam wa masuala ya filamu kutoka nchini Ujerumani Daniel Uphaus kwa kushirikiana na Sye ambaye ni mtaalamu wa kuongoza filamu.
Wataalu hao wameirekodi kwa makini albamu hiyo hali iliyopelekea kukubalika katika soko la kimataifa, ambapo tayari vituo vya Chanel O na Mtv Base wameiomba kwa ajili ya kuirusha katika runinga zao.
Ubora wa albamu hiyo ya The Best of David Robert umetokana na maandalizi ya miaka mitatu aliyoyafanya kabla ya kuchukua uamuzi wa kuingia studio na kutoa kitu hicho ambacho kinamvuto mkubwa.
Kukamilika kwa albamu hiyo kulichukua miezi minne na baada ya kurekodiwa aliipeleka kwa wataalam wengine kabla ya kuingia sokoni. Katika kuhakikisha albamu hiyo inakuwa tofauti na albamu nyingine hasa za muziki wa injili nchini, Robert alisafiri mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata picha nzuri kutokana na ujumbe wa nyimbo husika.
Mikoa aliyofanikiwa kwenda kurekodi albamu hiyo ni Morogoro, Iringa, Arusha, Moshi, Pwani na Dar es Salaam.
Aliyemvutia katika anga la muziki wa injili
Robert alisema kuwa huduma ya uimbaji alikuwa nayo tangu akiwa mtoto, ana alipokuwa shuleni huduma hiyo aliifanya kwa nguvu zote kwa kutembelea shule mbalimbali kwa lengo la kutoa injili ya njia ya nyimbo mwaka 1998 na kipindi hicho alikuwa akisoma shule ya sekondali Jitegemee ya jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kuipenda huduma hiyo, Mhungaji Elpham Mwansasu, Mchungaji Daniel Richard Mwansumbi na Cosmas Chidumule ndiyo waliompa hamasa kubwa Robert kujikita katika anga la muziki huo wa injili. Waimbaji hao ndio walikuwa wakimvutia kutokana na sauti zao kuwa nzuri pamoja na ujumbe wa nyimbo uliokuwemo ndani ya nyimbo hizo.
Mafanikio aliyoyapata kutoka na huduma ya uimbaji wa muziki huo
Kupitia muziki huo wa injili Robert amefaniki kujenga nyumba nzuri ya kisasa, ana gari nzuri. Mafaniko mengine alisema ni pamoja na kupata mtandao mzuri wa marafiki ndani na nje ya nchi na ana miradi mbalimbali inayomsaidia kuendesha maisha yake ya kila siku.
Matatizo anayokumbana nayo
Kuwa na mtaji mdogo wa kuitangaza huduma ya Mungu ndani na nje ya nchi, kutumia gharama kubwa katika kurekodi albamu na mwisho wa siku anajikuta mfukoni hana kitu.
Wito kwa wanamuziki wa injili hapa nchini
Anakerwa na waimbaji wanao kukimbilia katika muziki huyo kwa kuangalia pesa zaidi kuliko huduma. Ambapo watu wengi wamekuwa wakijikuta wanashindwa kufanya vema kazi ya Mungu pindi wanachokitarajia wanapokikosa.
Mwanamuziki anayemzimikia zaidi
Bila kificho David Robert alisema kuwa muimbaji mwenzake anayetamba na albamu ya Unikumbe Christina Shusho, ndiye anayemzimikia zaidi kutokana na nyimbo zake kuwa na ujumbe muzito ambao mara nyingi nyimbo hizo hugusa maisha anayopitia.
Matarajio yake ya baadaye
Ni kufanya mapinduzi makubwa katika muziki wa injili kwa siku za usoni. Mbali na hilo anatarajia kufanya uzinduzi wa albamu hiyo mwishoni mwa mwaka ujao. Je unamaoni gani kuhusu huduma ya David Robert? Usisite kunitumia maoni yako.
KABULA AIWEKA WAKUFU ALABAMU YAKE MPYA YA NITANG'ARA TU
Mwambaji
wa Injili nchini Mwinjilisti Kabula J.George amefanikiwa kutoa albamu
yake ya tatu ikijulikana kwa jina la Nitang'ara Tu. Albamu hiyo
aliiweka wafu hivi karibuni katika Huduma ya Neno la Upatanisho iliyopo
Kitunda Kivule jijini Dar es Salaam. Albamu hiyo itaingia sokoni hivi
karibuni.

Muonekano wa albamu ya Nitang'ara Tu kwa mbele.

Muonekano wa albamu hiyo kwa nyuma
Mchungaji Anna Suguye akiiweka wakufu albamu ya Nitang'ara Tu Mei 29,2011

Kabula na vijana wake wakiwa wanaomba wakati albamu hiyo ikiwekwa wakufu

Kabula akiwa katika hali ya maombi wakati wa kuiweka wakufu albamu yake mpya

Muonekano wa albamu ya Nitang'ara Tu kwa mbele.

Muonekano wa albamu hiyo kwa nyuma

Mchungaji Anna Suguye akiiweka wakufu albamu ya Nitang'ara Tu Mei 29,2011

Kabula na vijana wake wakiwa wanaomba wakati albamu hiyo ikiwekwa wakufu

Kabula akiwa katika hali ya maombi wakati wa kuiweka wakufu albamu yake mpya

Anastazia mkabwa kutoka Kenya.
Akimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji wa nyimbo za Injili ok swali kwako wewe uliye okoka unatumika vipi kwa Mungu.
Naye dada yangu Upendo Nkone naye anaonyesha kipaji chake alichopewa na Mungu swali tena kwako una kipaji gani na unakitumiaje, ?????????????????????????

Saturday, 18 January 2014
UPENDO & FURAHA
Huduma
Ya UPENDO & FURAHA ya jijini Dar es salaam, inatafuta vijana wa
Kikristo waliokoka, kwa ajili ya kuunda kwaya ya muziki wa injili
itakayokuwa ikihudumu katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na katika nchi
jirani.
SIFA ZA WATU WANAOHITAJIKA:-
i. Awe na karama ya uimbaji.
ii. Awe na umri wa kuanzia miaka 16 hadi 35.
iii. Awe ameokoka na mwenye hofu kuu ya Mungu.
iv. Awe na wito wa kweli wa kumtangaza na kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
v. Awe na utayari, pamoja na muda wa kutosha wa kusafiri na huduma katika mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na nchi jirani.
vi. Awe mkazi wa Dar es Salaam.Usaili utafanyika siku ya tarehe 06 Januari 2014.
MWISHO wa kujiandikisha ni tarehe 24 Desemba 2013.
Ili kujiandikisha, fikaofisini kwetu siku za kazi kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni, au wasiliana nasi kwa namba ya simu 0784406508.
HOT NEWSSS WAENDESHA BODABODA UYOLE WAKIMBIA NA MAITI YA MWENZAO BAADA YA MCHUNGAJI KUWAAMBIA WAMEFWATA UBWABWA
Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of
God[TAG]Uyole Njia Panda amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Waendesha
pikipiki[Bodaboda]kuvuruga ibada ya mazishi ya mwendesha pikipiki aitwaye
Gabriel Osward Ngalele.
Vurugu hizo zilitokea katika Kanisa hilo baada ya Gabriel
Ngalele kufariki kwa ajali ya gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la
SAE akiwa na abiria wake ambapo walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.
Taratibu za mazishi zilipokamilika mwili wa marehemu
ulipelekwa katika Kanisa hilo wakati mchungaji akiendesha Ibada aliomba utulivu
kwa wafiwa ambapo walitulia lakini vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda
walilipuka kwa kelele hali ilyomfanya mchungaji kuomba utulivu katika Ibada.
Hata hivyo vijana hao waliendelea kujaa katika kanisa hilo
na kukosekana utulivu hali iliyomlazimu mchungaji kuwaambia kama wamekosa
utulivu basi watakuwa wamefuata ubwabwa katika msiba huo hali iliyofanya
kutokea mtafaruku mkubwa.
Katika mtafaruku huo ilpelekea vijana kuuchukua mwili wa
marehemu hadi kwenye makaburi huku wakimwacha mchungaji ambapo ililazimu jeshi
la polisi kuingilia kati na kuzuia fujo kanisani na kuamua kumresha nyumbani
kwake kwa ulinzi mkali.
Wakati mchungaji akisindikizwa nyumbani kwake vijana
waliendelea na taratibu za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa
Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma huku mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote
akiendesha Ibada ya mazishi.
Katika mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali
walishiriki akiwemo mlezi wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius
Timanywa ambaye aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara
kwa mara.
Kwa upande wake mchungaji Edward Mtweve wa Kanisa la TAG
amesema amesikitishwa sana na kitendo cha kuvurugwa kwa Ibada kwani amesema
kuwa wengi wa waliokuwa wakifanya fujo walikuwa ni walevi na wavuta bangi na si
waumini wa Kanisa lake.
Aidha Mtweve na Baraza la wazee wamesema kuwa hawakusudii
kuchukua hatua zozote dhidi ya vijana ambao wamefanya fujo kwani yote
wanamwachia Mungu na kwamba katika kanisa hilo hakuna tukio lilowahi kutukia.
Pia amesema kitendo cha kuchukua mwili wa marehemu
madhabahuni ni cha utovu wa nidhamu kwani vijana wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu.
Wakikabidhi rambirambi kwa mjane ,Mwenyekiti wa Bodaboda
Jiji Vicent Mwashoma amesema pesa za rambirambi zitumike kusaidia familia ya
marehemu badala ya ndugu kutumia pesa hizo kuendeshea msiba huo.
wokovuimelda.blogsport.com
HISTORIA YAKE KIMUZIKI
IMELDA alianza kujishughulisha na maswala ya muziki mwaka 2012 lakini alianza lasmi uimbaji huo mwaka 2013 katika kanisa la E.A.G.T DEKAPOLI YA IGAWILO MBEYA.
Nilipo taka kufahamu nikwanini aliamua kuimba nyimbo za injili Imelida alisema kwama kwasababu huwa anapenda sana kumutumikia Mungu, na alisema anaguswa sana na nyimbo za Injili pia amekulia katika familia ya Kikristo ndipo alisema nilipo amua kumpokea Kristo hapo nilipogundua kuwa nini Mungu amenizawadia nami nikatumia zawadi hiyo kufanya kazi yake aliye nipeleka maadamu ni mchanga asipoweza mtu kufanya kazi.
Nilipo taka kufahamu nikwanini aliamua kuimba nyimbo za injili Imelida alisema kwama kwasababu huwa anapenda sana kumutumikia Mungu, na alisema anaguswa sana na nyimbo za Injili pia amekulia katika familia ya Kikristo ndipo alisema nilipo amua kumpokea Kristo hapo nilipogundua kuwa nini Mungu amenizawadia nami nikatumia zawadi hiyo kufanya kazi yake aliye nipeleka maadamu ni mchanga asipoweza mtu kufanya kazi.
NI MWIMBAJI CHIPUKIZI WA NYIMBO ZA INJILI, ANAYE TARAJIA KUKULETEA ALBAM MPYA IITWAYO JINA LIMETUKUKA, KUWA MACHO USIPITWE NA KIBAO HICHO KIJACHO HIVI PUNDE.
HISTORIA YAKE KIMAISHA
IMELDA ALIZALIWA MIAKA 22 ILIYOPITA KATIKA MKAO WA MBEYA NA KATIKA FAMILI YA KIKUHANI YA OSIAH SAKALANI IMELDA NI MTOTO WA 1 KATI YA WATOTO 5 KABILA LAKE NI MSAFWA KWA UPANDE WA BABA NA MNYACHUSA KWA UPANDE WA MAMA.
HISTORIA YAKE KIMAISHA
IMELDA ALIZALIWA MIAKA 22 ILIYOPITA KATIKA MKAO WA MBEYA NA KATIKA FAMILI YA KIKUHANI YA OSIAH SAKALANI IMELDA NI MTOTO WA 1 KATI YA WATOTO 5 KABILA LAKE NI MSAFWA KWA UPANDE WA BABA NA MNYACHUSA KWA UPANDE WA MAMA.
Wednesday, 15 January 2014
Kwa msaada wa Mungu tunashinda yote tunasonga mbele kwasababu yeye ni kiongozi wetu
mtengemee Mungu kwa kila jambo yeye anaweza kwa kila jambo MUNGU NI MWAMINIFU KWA KILA JAMBO
mtengemee Mungu kwa kila jambo yeye anaweza kwa kila jambo MUNGU NI MWAMINIFU KWA KILA JAMBO
HAKUNA KISICHO WEZEKANA KWA BWANA
- mtegemee mungu katika kila bambo utafanikiwa je unamtegemea nani katika maisha yako?
Mungu ni yule jana leo na hata milele ukimpa maisha yako kila utakacho hitaji kwake utapata je wahitaji nini kwa mungu// usisite yeye ndiye muumba wa vyote anaweza kukusaidia - Weka tumaini kwa bwana
Subscribe to:
Posts (Atom)