Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of
God[TAG]Uyole Njia Panda amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Waendesha
pikipiki[Bodaboda]kuvuruga ibada ya mazishi ya mwendesha pikipiki aitwaye
Gabriel Osward Ngalele.
Vurugu hizo zilitokea katika Kanisa hilo baada ya Gabriel
Ngalele kufariki kwa ajali ya gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la
SAE akiwa na abiria wake ambapo walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.
Taratibu za mazishi zilipokamilika mwili wa marehemu
ulipelekwa katika Kanisa hilo wakati mchungaji akiendesha Ibada aliomba utulivu
kwa wafiwa ambapo walitulia lakini vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda
walilipuka kwa kelele hali ilyomfanya mchungaji kuomba utulivu katika Ibada.
Hata hivyo vijana hao waliendelea kujaa katika kanisa hilo
na kukosekana utulivu hali iliyomlazimu mchungaji kuwaambia kama wamekosa
utulivu basi watakuwa wamefuata ubwabwa katika msiba huo hali iliyofanya
kutokea mtafaruku mkubwa.
Katika mtafaruku huo ilpelekea vijana kuuchukua mwili wa
marehemu hadi kwenye makaburi huku wakimwacha mchungaji ambapo ililazimu jeshi
la polisi kuingilia kati na kuzuia fujo kanisani na kuamua kumresha nyumbani
kwake kwa ulinzi mkali.
Wakati mchungaji akisindikizwa nyumbani kwake vijana
waliendelea na taratibu za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa
Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma huku mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote
akiendesha Ibada ya mazishi.
Katika mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali
walishiriki akiwemo mlezi wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius
Timanywa ambaye aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara
kwa mara.
Kwa upande wake mchungaji Edward Mtweve wa Kanisa la TAG
amesema amesikitishwa sana na kitendo cha kuvurugwa kwa Ibada kwani amesema
kuwa wengi wa waliokuwa wakifanya fujo walikuwa ni walevi na wavuta bangi na si
waumini wa Kanisa lake.
Aidha Mtweve na Baraza la wazee wamesema kuwa hawakusudii
kuchukua hatua zozote dhidi ya vijana ambao wamefanya fujo kwani yote
wanamwachia Mungu na kwamba katika kanisa hilo hakuna tukio lilowahi kutukia.
Pia amesema kitendo cha kuchukua mwili wa marehemu
madhabahuni ni cha utovu wa nidhamu kwani vijana wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu.
Wakikabidhi rambirambi kwa mjane ,Mwenyekiti wa Bodaboda
Jiji Vicent Mwashoma amesema pesa za rambirambi zitumike kusaidia familia ya
marehemu badala ya ndugu kutumia pesa hizo kuendeshea msiba huo.
wokovuimelda.blogsport.com
No comments:
Post a Comment