Saturday, 1 February 2014




 Nabii Flora

SALAMU ZA NABII FLORA
Ninawasalimu kwa jina la Yesu, ninawakaribisha katika kipindi kizuri cha neno na uzima, uponyaji na miujiza, wakati huu ni kipindi cha neno. Kabla sijaongea chochote nitaongea na Mungu kwaajili ya kumaliza mwezi huu mwezi Abuu, ambao anamwambia Nabii Ezekieli kwamba waambie watu wangu wana wa Israeli huu ni mwezi kwao wa Baraka, utakuwa ni mwezi kwao wa majibu.



KUOMBEA VIJANA AJIRA
Kabla sijaomba nimeambiwa na Mungu usiku wa leo kipindi tunamaliza mwezi nimeona kunavijana wanatamani ajira lakini hawana ajira. Baba wabariki vija kabla hatujamaliza mwezi, ulisema utaruhusu wingi wa Baraka za pesa, ajira, utajiri 1, 2, 3 vijana wote pokea.
 
 
 Ee Mungu uliyetukuka ninakwenda kuachilia upako wa ajira kwa vijana hawa, upako wa pesa wameshindwa wengine kuoa kwa sababu ya fedha wengine maisha yao yameyumba, wanalala wanakuwa kama wamechanganyikiwa Baba maisha yamekuwa magumu leo naachilia wingu la Baraka, naziinamisha mbingu juu yenu 1, 2, 3 tooouuuchhhh


Baba nahitaji vijana hawa wakusujudie maana umesema  wakuabuduo watakuabudu katika Roho na kweli, Baba nahitaji watu hawa uwabariki Mungu, nafungua kamba mikononi mwenu, kuna watu wamekamata pesa azikai mpo hapa nataka leo mumsujudie huyu Mungu aliyetamalaki katika matuo haya wote sujudu pokea. Kwa Damu ya Yesu Kristo ulisema kila goti litapigwa asema Bwana na kila ulimi utakiri, sujudu mbele za Bwana Mungu wa majeshi.



KIPINDI CHA MAOMBEZI NA UPONYAJI
Hawa ni watumishi wa Mungu tena aliye hai, tunamtangaza Mungu aliye hai, kwa neno la ufunuo ishara na miujiza iliwatupeleke mbinguni kwa yeye aliye hai. Nipo hapa kwaajili ya kusogeza kupeleka juu ya meza kuu kwake yeye aliye hai, lazima tumjue Mungu wa kweli ndipo tuweze kufanikiwa. Lazima tumjue Mungu anayetenda, watumishi wakipakwa mafuta wanapaswa kuheshimiwa.
 

Nasema na watu pokea nakufungua vifungo vyako, umekaa mwezi mzima ujapata pesa toka mwaka umeingia leo ni miezi mitano hujafanikiwa leo ni siku yako ya kufanikiwa, pokea baraka nasema pokea. Nazungumza na watu mnaoniangalia, wageni mbalimbali nasema pokea wafanya biashara nasema na ninyi leo.



Nasema kuna watu wamefungwa vifungo kichwani wanasikia sauti za ajabu, umekuwa ukisikia sauti inakwambia utakufa, nakutamkia haufi. Pokea baraka sasa, kuna watu wenye Kansa, Ukimwi leo uponyaji unaingia, pokea kupona  wewe mwenye pepo la Ukimwi pepo la Kansa nakufuatili kwa moto mkali nakukausha achilia watu sasa, oooh Yesu nakuita nakuita Baaba leo ninakausha Ukimwi watu elfu moja mia tano wanakwenda kupima watakuta negative.


Kuna watu wanamajini mahaba yamekufunga hupati kazi, huolewi nasema inuka  umekuwa ukifanya mapenzi na mtu usiyemjua, yapo majini mahaba yanatoka wengine virusi vya Ukimwi leo vinatoka. Yesu anatembea lazima atembee kwako leo tunakwenda kuingia mwezi mpya, nakwambia ruka kamba zako zinakwenda kukatika leo pokea nafasi ya kuwa mkurugenzi lazima upate.



Lazima tugawe mwaka na baraka zetu hujaolewa utakwenda kuolewa, hujapata mtoto hutapata mtoto, hujapokea ujauzito utapokea, nasema na watu wenye masikio. Ninakuapia kw ajina la Yesu mwanao atasoma shule kama kulikuwa na mtu anamloga hata mloga tena, nasema nikiwa na uhakika na Mungu ninaye mtumikia, Mungu wangu ni Mungu anayeona.



Lazima tuvuke mwezi wa sita na vitu vyetu, waume zetu, wake, watoto, ng’ombe lazima tuvuke na baraka na upako wetu. Baba zibitisha neno hili kwa ishara watu hawa sikia manukato hapa, naigeuza hewa ya mahali hapa na pia watu hawa wapigwe tiki wengine waone baraka mikononi mwao. Na pia hewa geuka unayenisikia hewa ya mahali hapa nakugeuza ugeuke kuwa baraka, watu wavutapo hewa hii wapokee mafanikio naseama hewa geuka kuwa manukato mazuri na kuwa baridi na kuwa mafanikio, naamuru mafanikio madhabahu toa moto nasema hewa geuka.
Hii ni huduma ya maombezi maana yake manukato, katika Ufunuo 5:8, nasema Bwana tembea katika huduma hii ya manukato naigeuza hewa nasema hewa geuka watu wapokee manukato, watasikia manukato mazuri  ooh Yesu tembea na kuwa manukato mazuri. Hata mtumishi wa Mungu Rulea Sanga apokee Baraka juu ya kazi zake Yesu akuinue pokea manukato mazuri.
 Oooh Baba tembea umetukuka Jehova umetukuka naigeuza hewa, maana ya manukato ni maombi yetu yamepewa kibali mbele za Mungu, wagonjwa wa Ukimwi wameponywa, mkansa zimeponywa, maana ya manukato utasoma katika Ufunuo. Andiko limeandika katka Ufunuo nikaona chetezo moshi ukatanda wa arufu nzuri hayo ni maombi ya watakatifu.
 Ufunuo 8:3
Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu akapewa uvumba mwingi iliautie pamoja na maombi ya watakatifu juu ya madhabahu ya dhahbu iliyo mbele ya kiti cha enzi. Malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi iliautie pamoja na maombi ya watakatifu juu ya madhabahu ya dhahabu iliyombele ya kiti cha enzi. Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu.
Sikumoja niliona moshi unapanada chumbani kwangu unakwenda juu nikasikia sauti inaniambia maombi yako yamekubalika mbele za Bwana, yamekuwa manukato mbele za Mungu. Kumbe ule moshi ukipanda juu ni manukato mbele za Mungu, ukiona unaomba tu moshi unatokea jua anayekuongoza amekubaliwa na Mungu.
UJUMBE WA LEO UTATOKA KATIKA KITABU CHA YOELI
Yoeli 2:21-27
Ee nchi usiogope furahi na kushangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu, msiogope enyi wanyama wa kondeni maana malisho ya jangwani yanatoa miche ; anasema ee nchi shangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu tangu mwezi wa kwanza hadi huu wa tano. Hata kama uchumi wako ulikuwa umekauka, nyumbani kwako kulikuwa na jangwa katika mwezi huu Abuu lazima mimea yako itatoa miche, palipo kuwa na jangwa patatoa maji, ulikuwa imesimamishwa kazi utarudishwa kazini, ulikuwa huapata promotion utapata, anasema enyi nchi furahi sana na kushangilia kwa kuwa tazama mimea inatoa miche palipo na jangwa lakini hasubuhi ya leo patakuwa na baraka.
Hata kama ulikuwa na ukame  wa fedha Bwana ataruhusu baraka za pesa  zitakuja kwako, nasema pokea kabla hatujavuka mwezi. Yesu atafanya kitu kwako zipo siku nne mbele akaunti zako utazikuta zimejaa, ikiwayule baba muhaya amepata laki saba wiki hii iweje wewe usipae, anasema nchi usiogope ujapotishwa ukaambiwa  utasimamishwa kazi usiogope nchi tazama malisho ya kondeni yanatoa miche hata nyie wanyama wa kondeni msiogope maana palipo na jangwa patatoa maji siku ya leo.
Na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu unatoa nguvu zake; maana ya mti ni mtu yaani wewe mwanadamu uliyefika mahali hapa utazaa matunda yake, utakuwa kama mti uliopandwa katika vijito vya maji tena uzaao matunda kwa majira yake. Nakutamkia kufanikiwa, nakutamkia kuwa kama mti ulipandwa katika vijito vya maji unakwenda kuvuka mwezi mwingine, nataka Mungu akutendee wewe, lazimaMungu aruhusu baraka kwako zitoke za kila aina.
Ujapo kaa miezi mi tano hujafanikiwa usiogope ewe Mtanzania, furahia na kushangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu leo. Lazima Bwana atatenda kwako mambo makuu, pakiwa na ukame pataamuriwa maji kutoka anasema na mti utatoa matunda yake yaani familia yako inakwenda kutoa baraka za kila aina leo, nakupa ufunguo wa baraka hujaolewa nakupa funguo ya kuolewa, hujaendesha gari nakupa funguo ya gari, hujapata mtoto nakukabidhi funguo wa mtoto pokea sasa furahi na kushangilia.
Yaani tarajia kabisa leo hii ukitoka hapa maisha yako yatakwenda kufunguliwa. Nakuapia kwa jina la Yesu lile jiwe litabiringishwa asema Bwana wa majeshi, lazima huinuke, hufanikiwe kiuchumi lazima maisha yako yabadilike. Uliyefika hapa umetumia nauli Yesu azihesabu hatua zako akubariki wewe uliyefika hapa lazima Yesu atende mambo makuu.kumbe katika mzabibu pia kunanguvu, ndio maana watu tunawapa mzabibu. Yesu alisema yeye ni mzabibu wa kweli anywae mzabibu na kuinywa  Damu yake ataona mauti naye atafanikiwa na kustawi sana .
Na kwambia haijalishi watu wamefunga  mambo yako, ulikuwa unapafomu vizuri shuleni sasa virus amekula nakutamkia ukitoka hapa mambo yako yatakuwa safi. Usiogope nchi furahi na kushangilia kwa kuwa Bwana  ametenda mamboa makuu. Haijalishi umefungwa tumbo lako toka mwezi wa kwanza hadi mwezi wa tano hujajibiwa, nakwambia mti huu utatoa nguvu zake na mzabibu huu utatoa nguvu zake.
Lazima watu wafunguliwe leo, ninaona vijana wanaangaika hawana ajira, watu wanakula chakula cha shida na kulala kwa shida leo nakutamkia hadui zako waliweka ukuta nitauporomosha lazima uvuke, nikutoe ng’ambo nikuvushe katika mto Neriba.
Furahini basi enyi wana wa Sayuni  mkamfurahiye Bwana Mungu wenu; watu wamepona vipofu wameona, watu wamepona Ukimwi anasema enyi wana wa Sayuni furahini basi, napenda kuona watu wakifurahi asubuhi ya leo ebupokea baraka za kufurhi sasa, anasema furahini na kushangilia kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu.
Kwa kuwa ninyi huwapa mvua tena kipimo cha haki, huwapa ninyi mvua ya masika kwa kipimo cha haki,  Naye uwanyeshea mvua, mvua ya masika na mvua ya vuli; nataka Bwana akupe kipimo cha haki Yesu akupe baraka usibaki chini kijana Yesu akupe kipimo cha haki. Maana ya mvua ni Baraka, anaseama atawanyeshea mvua kama kwanza yaani ataziruhusu baraka kama hapo kwanza, kama ulikuwa na maduka ukafilisika tarajia kuibuka, ulikuwa na cheo kikubwa tarajia kupandishwa, ilikuwa milango imefungwa tarajia kupata pesa pokeaaaa! kwa  jina la Yesu.
Naachilia fataki watu waponywe leo, watu wamefurahiya na kushangilia kwa kuwa Mungu ametenda mambo makuu, hupo hapa mama umefungwa na wachawi hupati mtoto nalifungua tumbo lako pokea  funguka leo, majini mahaba yanaondoka, mchumba aliyekuacha anakurudia, mume wako anarudi, nafasi ya kazi inarudi mshahara unaongezewa.
Yamkini wewe umekuwa hupati mafanikio, unasikia sauti kichwani mwako inakwambia ondoka hapa acha kazi hilo nipepo leo nalitoa 1, 2, 3 tooouuuuchhhh! Pokea funguka watu , nasema na watu leo. Kuna watu hapa mambo yao hayaendi  biashara zimeyumba , wengine wana presha, kisukari, Ukimwi, wengine wamefukuzwakazi, wengine hawana mitaji, wengine Mungu wamezarauliwa bila sababu leo Bwana anasema furahi na kushangilia kwa kuwa Yesu anatenda mambo makuu.
Unawatoto wako shuleni hawafanikiwi wakisoma wanafeli, nakwenda kuangusha achia watu hawa 1, 2, 3 pokea kwa  jina la Yesu naachilia mlipuko. Nasema lipo pep[o ndani mwako leo naling’oa inuka jinni mahaba tooka achia watu wanafunguliwa leo.  Mme wako alikuwa alali nyumbani leo atalala nyumbani, hupati pesa leo utapata pesa, hauna mtaji pokea mtaji.
Na sakafu za kupeetea zitajaa zitajaa ngano na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta; mama unavyombo vyoko, masinia Bwana anakwenda kujaza baraka, nyumba yako itajaa baraka sasa tunavuka na utajiri wetu. Nataka tunapoingia mwezi wa sita tunatoka na baraka zetu  watu wakajae kiuchumi, kifedha pokea sasa kumiliki Baraka.
Baba watu hawa wapo tayari asubuhi ya leo kujazwa hazina zao, mashinikizo yao wameinua mikono wanahitaji Mungu ujaze akaunti zao, ujaze kazi zao, ujaze nyumba zao baraka. Nasema na watu wanao nitazama kwenye yuotube, wanaonisoma kwenye blogu na facebook na waliofika hapa matuo haya kwamba wiki ijapo itakuwa ni mwezi mpya nitakwambia mwezi unasimamia nini.
Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige na hata ile iliyoliwa na parare na ile iliyoliwa na madumadu na maturutu ; yamkii baba au mama, kijana upo hapa lakini kuna miaka yako iameliwa na nzige umefanya biashara ulikuwa na maduka kariakoo, ulikuwa na maduka mwenge ya vinyago ulikuwa na wateja wazungu leo wamekukimbia wote sasa nakurudishia wale wateja wa vinyago wazungu kutoka Marekani. Nakurudishia leo ile miaka yako iliyoliwa na nzige pokea sasa wateja.
Yamkini mama ulikuwa na miaka ya mafanikio, mlikuwa mkipanga mipango mkiwa hanimoni kitandani vizuru mnaelewana lakini madumadu kala mwaka wenu, maturutu kashambulia ndoa yenu sasa hivi mnalala mvungu wan ne mwanaume amevaa jinsi sita mwanamke night dres saba, leo Bwana anakwenda kurejesha amani, anakwenda kurejesha miaka yenu katika vitanda vyenu.
Nanyi mtakula chakula chenu na kushiba; anasema Bwana nasi tutakula chakula tele tena na kushiba, Bwana anakwenda kutupa kushiba wewe ambaye unakula robo kilo kwa sababu ya bajeti pesa zimeyumba Bwana anafungua milango ya pesa leo naifungua sasa kwako, nasema pokea milango ya pesa naifungua sasa utakula na kushiba Yesu atajaza.
Na kuliimidi jina la Bwana Mungu wenu aliye watendea mambo makuu; nataka watu waliimidi jina la Bwana, kama hupo hapa kunamchawi alikuloga alikuendea Bagamoyo, Kigoma mwishop wa reli, ameenda Sumba wanga, Nigeria amekuloga nakwambia hapa imesimili kabisa hapa ngoma imedunda mwambie amechemka. Yule Nabii akasema kwa kinywa cha Bwana kwamba popote walipokuwa wametufunga tumekwisha kufunguliwa.
Nanyi mtajua mimi ni katikati ya Israeli na yakuwa mimi ndimi Bwana Mungu wenu, wala hakuna Mungu mwingine na watu wangu hawata tahayari kamwe; haijalishi chochote umenenewa wamesema mwanao hata soma ninakutamkia mwanao lazima asome, hata kama mchawi atakuwa dirishani kwako lazima atainamishwa anashushwa kama mpira asema Bwana wa majeshi lazima wewe ufanikiwe.
KUOMBEA VITAMBAA
Petro mtume aliponya wagonjwa kupitia vitambaa, nataka mikono yako kila utakapogusa kitambaa upate mafanikio, palipo na giza patakuwa na nuru, tunaingia mwezi wa sita mwezi  ambao nitakupa jina lake unaitwa Eluli yaani mwezi wa kutokewa. Kama hujawahi kutokewa na malaika utatokewa mwezi wasita, hujawahi kusikia sauti ya Mungu utaisikia. Nataka ukamate kitambaa cheupe kuashiria nyumba yako kama kulikuwa kunagiza linakwenda kutoka. Baba tazama tendo hili la utukufu la kusisimua na la kushangaza, maajabu na miujiza ambalo Baba Mungu mbingu zimeikubali, Mungu umekubali kutoka mbinguni mtume Petro na Yohana waliponya watu kupitia leso zao na mimi Baba nimewamilikisha vipawa, nimewapa vitambaa vyeupe kinaashiria utukufu wa Mungu. Maana ya kitambaa cheupe ni utukufu, ukamwingie kila mmoja utukufu palipokuwa na giza giza liondoke, maana Mungu amesema tazama nuru yang’ara gizani na giza halikunishinda . nami ninasema kupitia vitambaa hivi mambo yako yote yanakwenda kufunguka, palipo kuwa pagumu patafanywa kuwa pepesi.
Nuru ikuangazie Pasta Ansila, Watumishi wa Mungu, Yesu akafungue mbingu nasema kitambaa hiki kitakuwa Baraka ndani ya maisha yako asubuhi shika na jioni hadi siku 21 utaona mambo yako yanafunguka. Wasio kusalimia watakusalimia, utakanyaga sehemu isiyo kanyagika napo utapata kibali natamka baraka sasa ninaachilia na tunaondoka na Baraka zetu za mwezi wa kwanza, wa pili, wa tatu, wan ne, wa tano tunavuka nazo mto Yordani. Kwani miaka yetu iliyoliwa na nzige tumerejeshewa, muzuri wetu umerejeshwa, maisha yetu marefu yamerejeshwa, tumerejeshewa utajiri, watoto, vibali makazini, vyeo, afya zetu CD4 zilizoshuka wapendwa zimerejeshwa kwa Damu ya Yesu.

SHUKRANI
Baba tumejionea kwa macho yetu na tumesikia kwa masiko yetu, nasi Baba sifa na utukufu tunakurudishia wewe, na tunakuomba Mungu wetu endelea kumtumia mtumishi wako Nabii Flora kuwatendea wengine ambao hawaja shuhudia ili Mungu waweze kushuhudia kile ulicho watendea katika jina la Yesu ninaomba na kushukuru Amen.
Tembelea: 



MAOMBI NA KUABUNDO NI MHIMU SANA KWA MCHRISTO MAANA NDO NJIA YA KUONGEA NA MUNGU WETU HIVYO, OMBENI BILA KUKOMA MAANA UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA ASANTE. MUNGU AWABARIKI SANA

MZEE WA UPAKO AVAMIWA

Mzee wa Upako


Haruni Sanchawa na Gladness Mallya

MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi – Utashinda, Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako usiku wa kuamkia jana alivamiwa kanisani na kundi la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kumteka kwa muda kabla ya kumpora mamilioni ya shilingi.

Gazeti hili lilifika eneo la tukio kanisani kwake, maeneo ya Ubungo Kibangu na kufanikiwa kupewa taarifa ya jinsi ujambazi huo ulivyofanyika ambapo mtoa habari alisema kundi la majambazi lilivamia kanisa hilo usiku.

“Kundi hilo la watu lilifika maeneo hayo majira ya saa tisa na kuwateka walinzi ambao walikuwepo hapo hadi saa kumi na moja alfajiri kuamkia jana,” alisema mtoa habari wetu kwa sharti la kutoandika jina lake gazetini.

Imedaiwa kuwa kabla ya kufanya uvamizi huo, mlinzi wa kanisa hilo (jina tulihifadhi kwa sababu za kiusalama ), alivamiwa na kufungwa kamba na baadaye kunyang’anywa bunduki na majambazi hao.

Chanzo chetu hicho cha habari kiliongeza kuwa baada ya kumkamata mlinzi huyo, majambazi hao walienda moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Lusekelo na kumteka kwa muda kabla ya kumuamuru atoe pesa alizokuwanazo vinginevyo wangemuua.

Habari zinasema Mzee wa Upako aliamua kutoa pesa ambazo inadaiwa ni zaidi ya shilingi milioni 20 ambazo inaaminika zilitokana na sadaka za waumini wake. Kiongozi huyo wa kanisa hakujeruhiwa.

Habari za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa Mchungaji Lusekelo hakai kanisani hapo na kwamba ni mara chache hulala katika nyumba hiyo ya ibada hasa anapokuwa na kazi maalum.

Gazeti hili lilipowasiliana na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga alikiri kutokea kwa tukio hilo na amedai kuwa hadi sasa watu wawili wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.

“Uzoefu unaonyesha kuwa kuna baadhi ya makampuni ya ulinzi hapa nchini yana watumishi ambao si waaminifu, natoa wito kwa wamiliki wa makampuni binafsi ya ulinzi kabla ya kuajiri mlinzi , yahakikishe uaminifu wake kwanza,” alisema Kalinga.

Aliongeza kuwa kampuni za ulinzi zinalinda mamilioni ya mali za watu lakini anashangazwa kuona baadhi ya walinzi wao wanauza siri za muajiri wao kwa watu wasio raia wema.

Waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta Mzee wa Upako ili kusikia kauli yake juu ya tukio hilo bila mafanikio.
Kwa mujibu wa walinzi waliokutwa kanisani hapo ambao hawakupenda majina yao kuandikwa gazetini, kiongozi huyo alikuwa amekwenda nyumbani kwake Mbezi kupumzika.


Source:wokovuimelda.blogspot.com/
NI KITABU NINACHO KUPATIA UFAFANUZI KUHUSIANA NA WOKOVU KAMILI,  KWA MAANA KUNA WATU AMBAO WANAJIITA WAMEOKOKA NA KUMBE WAMAONGOKA, JIPATIE NAKALA YA KITABU HIKI UJIFUNZE WOKOVU KAMIRI BARIKIWA NA BWANA

oyoooooooooooooooooooooo

HATA KUTAKIANA HALI TU NI SAHIHI

Saturday, 25 January 2014

AVID ROBERT ANAYETARAJIA KUFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA MUZIKI WA INJILI TANZANIA “ Miaka ya nyuma muziki wa injili ulidharaulika sana na mtu alipoonekana akiimba muziki huo alionekana kama kituko fulani hivi kwa sababu hakuna aliyekuwa anaguswa na nyimbo hizo. Sio kwamba kipindi hicho hapakuwa na waimbaji wazuri wa muziki huo, la hasha! Walikuwepo tena wakali pengine kuliko waimbaji wa leo wanao mwimbia Mungu nyimbo za injili. Miaka hiyo kulikuwa na waimbaji kama Epharaem Mwansasu, Faustini Munishi, Mungu Four, Ency Mwalukasa, Jenifa Mgendi na miaka ya hivi karibuni alijitokeza Cosmas Chidumule aliyekuwa anapiga muziki wa dunia. Na miaka hiyo ilikuwa ni mara moja sana kusikia muziki wa injili kukipingwa katika kumbi za starehe kama bar, kwenye harus nk. Lakini leo hii upepo umebadilika,”. Ndivyo alivyoanza kusema nami mwanamuziki mahiri wa muziki wa injili nchini David Robert aliyeibuka katika anga la muziki huo mwaka 2002 na albamu ya Baba. Katika albamu hiyo Robert ambaye ana sauti nzito alishilikiana vema na Godwin Gondwe ambaye naye anasauti ya zege na kuifanya albamu hiyo kuwa na muvuto wa pekee na kuweka imara katika anga la muziki huo. Albamu hiyo iliyokuwa ni nyimbo kumi iliwashika wengi na kila mmoja kupenda kuzisikiliza. Nyimbo zilikokuwa katika albamu hiyo ni Baba, Niongoze, Ngulujangu (kinyakyusa), Nakupenda, Hosana, Tufani, Mimi nani?, Bwana atafanya njia na We njoo. Kufanya vizuri sokoni kwa albamu hiyo kulikuwa kama kumemtoa tongotongo machoni Robert. Kwani mwaka 2003 alilazimika tena kuingia studio na kufyatua albamu ya pili inayojulikana kwa jina la Kiganjani pa Mungu. Albamu hiyo nayo imewakamata vema wapenzi wa muziki huo na kuanza kumtaka arekodi mkanda wa video ili iwe rahisi kwao kuwa wanamuona kwa njia hiyo japo wako naye mbali. Albamu ya Kiganjani pa Mungu ilikuwa na nyimbo 8 ambao ni Neema, Sema nami, Shukurani, Nitakumbuka, E Yesu, Yesu ni Mungu na Kiganjani pa Mungu unaobeba albamu. Hakuna asiyeelewa kila kitu kinachotengezwa kwa ubora, hutumia gharama kubwa kukikamilisha. Mwimbaji huyo alilitambua hilo baada ya kuona wapenzi wa muziki wake kumtaka arekodi hizo katika mtindo wa video. Hata hivyo Robert alikaa na kutafari, kwa makini jinsi gani anaweza kurekodi video ambayo inaweza kuwa tofauti na video zilizotangulia. Jibu lake lilionekana kuwa ni kujiweka sawa katika fungu la fedha. Robert aliamua kuzichambua nyimbo zilizo katika albamu hizo mbili na kufanikiwa kurekodi albau moja aliyoipa jina la The Best Of David Robert ambayo tayari iko sokoni kuanzia wiki iliyopita na inapatikana kwa njia ya HVS, DVD, na VCD. Mwanamuziki huyo alisema kuwa albamu hiyo imerokodiwa katika madhari nzuri na mtaalam wa masuala ya filamu kutoka nchini Ujerumani Daniel Uphaus kwa kushirikiana na Sye ambaye ni mtaalamu wa kuongoza filamu. Wataalu hao wameirekodi kwa makini albamu hiyo hali iliyopelekea kukubalika katika soko la kimataifa, ambapo tayari vituo vya Chanel O na Mtv Base wameiomba kwa ajili ya kuirusha katika runinga zao. Ubora wa albamu hiyo ya The Best of David Robert umetokana na maandalizi ya miaka mitatu aliyoyafanya kabla ya kuchukua uamuzi wa kuingia studio na kutoa kitu hicho ambacho kinamvuto mkubwa. Kukamilika kwa albamu hiyo kulichukua miezi minne na baada ya kurekodiwa aliipeleka kwa wataalam wengine kabla ya kuingia sokoni. Katika kuhakikisha albamu hiyo inakuwa tofauti na albamu nyingine hasa za muziki wa injili nchini, Robert alisafiri mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata picha nzuri kutokana na ujumbe wa nyimbo husika. Mikoa aliyofanikiwa kwenda kurekodi albamu hiyo ni Morogoro, Iringa, Arusha, Moshi, Pwani na Dar es Salaam. Aliyemvutia katika anga la muziki wa injili Robert alisema kuwa huduma ya uimbaji alikuwa nayo tangu akiwa mtoto, ana alipokuwa shuleni huduma hiyo aliifanya kwa nguvu zote kwa kutembelea shule mbalimbali kwa lengo la kutoa injili ya njia ya nyimbo mwaka 1998 na kipindi hicho alikuwa akisoma shule ya sekondali Jitegemee ya jijini Dar es Salaam. Pamoja na kuipenda huduma hiyo, Mhungaji Elpham Mwansasu, Mchungaji Daniel Richard Mwansumbi na Cosmas Chidumule ndiyo waliompa hamasa kubwa Robert kujikita katika anga la muziki huo wa injili. Waimbaji hao ndio walikuwa wakimvutia kutokana na sauti zao kuwa nzuri pamoja na ujumbe wa nyimbo uliokuwemo ndani ya nyimbo hizo. Mafanikio aliyoyapata kutoka na huduma ya uimbaji wa muziki huo Kupitia muziki huo wa injili Robert amefaniki kujenga nyumba nzuri ya kisasa, ana gari nzuri. Mafaniko mengine alisema ni pamoja na kupata mtandao mzuri wa marafiki ndani na nje ya nchi na ana miradi mbalimbali inayomsaidia kuendesha maisha yake ya kila siku. Matatizo anayokumbana nayo Kuwa na mtaji mdogo wa kuitangaza huduma ya Mungu ndani na nje ya nchi, kutumia gharama kubwa katika kurekodi albamu na mwisho wa siku anajikuta mfukoni hana kitu. Wito kwa wanamuziki wa injili hapa nchini Anakerwa na waimbaji wanao kukimbilia katika muziki huyo kwa kuangalia pesa zaidi kuliko huduma. Ambapo watu wengi wamekuwa wakijikuta wanashindwa kufanya vema kazi ya Mungu pindi wanachokitarajia wanapokikosa. Mwanamuziki anayemzimikia zaidi Bila kificho David Robert alisema kuwa muimbaji mwenzake anayetamba na albamu ya Unikumbe Christina Shusho, ndiye anayemzimikia zaidi kutokana na nyimbo zake kuwa na ujumbe muzito ambao mara nyingi nyimbo hizo hugusa maisha anayopitia. Matarajio yake ya baadaye Ni kufanya mapinduzi makubwa katika muziki wa injili kwa siku za usoni. Mbali na hilo anatarajia kufanya uzinduzi wa albamu hiyo mwishoni mwa mwaka ujao. Je unamaoni gani kuhusu huduma ya David Robert? Usisite kunitumia maoni yako.

KABULA AIWEKA WAKUFU ALABAMU YAKE MPYA YA NITANG'ARA TU

Mwambaji wa Injili nchini Mwinjilisti Kabula J.George amefanikiwa kutoa albamu yake ya tatu ikijulikana kwa jina la Nitang'ara Tu. Albamu hiyo aliiweka wafu hivi karibuni katika Huduma ya Neno la Upatanisho iliyopo Kitunda Kivule jijini Dar es Salaam. Albamu hiyo itaingia sokoni hivi karibuni.

Muonekano wa albamu ya Nitang'ara Tu kwa mbele.

Muonekano wa albamu hiyo kwa nyuma
Mchungaji Anna Suguye akiiweka wakufu albamu ya Nitang'ara Tu Mei 29,2011


Kabula na vijana wake wakiwa wanaomba wakati albamu hiyo ikiwekwa wakufu


Kabula akiwa katika hali ya maombi wakati wa kuiweka wakufu albamu yake mpya













Anastazia mkabwa kutoka Kenya.
Akimtumikia Mungu kwa njia ya  uimbaji wa nyimbo za Injili  ok  swali kwako wewe uliye okoka unatumika vipi kwa Mungu.


Naye dada yangu Upendo Nkone naye anaonyesha kipaji chake alichopewa na Mungu swali tena kwako una kipaji gani na unakitumiaje, ?????????????????????????















Anajiita sauti ya asali Upendo kilahiro  haye hachezi mbali na Mungu chezea Mungu wewe akisema anainua kweli anainua




Saturday, 18 January 2014

UPENDO & FURAHA

Huduma Ya UPENDO & FURAHA ya jijini Dar es salaam, inatafuta vijana wa Kikristo waliokoka, kwa ajili ya kuunda kwaya ya muziki wa injili itakayokuwa ikihudumu katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na katika nchi jirani.

SIFA ZA WATU WANAOHITAJIKA:-

i. Awe na karama ya uimbaji.
ii. Awe na umri wa kuanzia miaka 16 hadi 35.
iii. Awe ameokoka na mwenye hofu kuu ya Mungu.
iv. Awe na wito wa kweli wa kumtangaza na kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
v. Awe na utayari, pamoja na muda wa kutosha wa kusafiri na huduma katika mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na nchi jirani.
vi. Awe mkazi wa Dar es Salaam.
Usaili utafanyika siku ya tarehe 06 Januari 2014.

MWISHO wa kujiandikisha ni tarehe 24 Desemba 2013.
Ili kujiandikisha, fikaofisini kwetu siku za kazi kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni, au wasiliana nasi kwa namba ya simu 0784406508.

HOT NEWSSS WAENDESHA BODABODA UYOLE WAKIMBIA NA MAITI YA MWENZAO BAADA YA MCHUNGAJI KUWAAMBIA WAMEFWATA UBWABWA



Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole Njia Panda amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Waendesha pikipiki[Bodaboda]kuvuruga ibada ya mazishi ya mwendesha pikipiki aitwaye Gabriel Osward Ngalele.

Vurugu hizo zilitokea katika Kanisa hilo baada ya Gabriel Ngalele kufariki kwa ajali ya gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la SAE akiwa na abiria wake ambapo walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.

Taratibu za mazishi zilipokamilika mwili wa marehemu ulipelekwa katika Kanisa hilo wakati mchungaji akiendesha Ibada aliomba utulivu kwa wafiwa ambapo walitulia lakini vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda walilipuka kwa kelele hali ilyomfanya mchungaji kuomba utulivu katika Ibada.

Hata hivyo vijana hao waliendelea kujaa katika kanisa hilo na kukosekana utulivu hali iliyomlazimu mchungaji kuwaambia kama wamekosa utulivu basi watakuwa wamefuata ubwabwa katika msiba huo hali iliyofanya kutokea mtafaruku mkubwa.

Katika mtafaruku huo ilpelekea vijana kuuchukua mwili wa marehemu hadi kwenye makaburi huku wakimwacha mchungaji ambapo ililazimu jeshi la polisi kuingilia kati na kuzuia fujo kanisani na kuamua kumresha nyumbani kwake kwa ulinzi mkali.

Wakati mchungaji akisindikizwa nyumbani kwake vijana waliendelea na taratibu za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma huku mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi.

Katika mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo mlezi wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius Timanywa ambaye aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.

Kwa upande wake mchungaji Edward Mtweve wa Kanisa la TAG amesema amesikitishwa sana na kitendo cha kuvurugwa kwa Ibada kwani amesema kuwa wengi wa waliokuwa wakifanya fujo walikuwa ni walevi na wavuta bangi na si waumini wa Kanisa lake.

Aidha Mtweve na Baraza la wazee wamesema kuwa hawakusudii kuchukua hatua zozote dhidi ya vijana ambao wamefanya fujo kwani yote wanamwachia Mungu na kwamba katika kanisa hilo hakuna tukio lilowahi kutukia.

Pia amesema kitendo cha kuchukua mwili wa marehemu madhabahuni ni cha utovu wa nidhamu kwani vijana wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu.

Wakikabidhi rambirambi kwa mjane ,Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma amesema pesa za rambirambi zitumike kusaidia familia ya marehemu badala ya ndugu kutumia pesa hizo kuendeshea msiba huo.

Na Emelda Sakalani
wokovuimelda.blogsport.com

HISTORIA YAKE KIMUZIKI


IMELDA alianza kujishughulisha na maswala ya muziki mwaka 2012 lakini alianza lasmi uimbaji huo mwaka 2013 katika kanisa la E.A.G.T DEKAPOLI YA IGAWILO MBEYA.


Nilipo taka kufahamu nikwanini aliamua kuimba nyimbo za injili Imelida alisema kwama kwasababu huwa anapenda sana kumutumikia Mungu, na  alisema anaguswa sana na nyimbo za Injili pia amekulia katika familia ya Kikristo ndipo alisema nilipo amua kumpokea Kristo hapo nilipogundua kuwa  nini Mungu amenizawadia nami nikatumia zawadi hiyo kufanya kazi yake aliye nipeleka maadamu ni mchanga asipoweza mtu kufanya kazi.
NI MWIMBAJI CHIPUKIZI WA NYIMBO ZA INJILI,  ANAYE TARAJIA KUKULETEA ALBAM MPYA IITWAYO  JINA LIMETUKUKA,  KUWA MACHO USIPITWE NA KIBAO HICHO KIJACHO HIVI PUNDE.

HISTORIA YAKE KIMAISHA 

IMELDA ALIZALIWA MIAKA 22 ILIYOPITA KATIKA MKAO WA MBEYA NA KATIKA FAMILI YA KIKUHANI YA OSIAH SAKALANI  IMELDA NI MTOTO WA 1 KATI YA WATOTO 5 KABILA LAKE NI MSAFWA KWA UPANDE WA BABA  NA MNYACHUSA KWA UPANDE WA MAMA.




Wednesday, 15 January 2014

WOKOVUIMELDA:

WOKOVUIMELDA:
Kwa msaada wa Mungu tunashinda yote tunasonga mbele kwasababu yeye ni kiongozi wetu
mtengemee Mungu kwa kila jambo yeye anaweza kwa kila jambo
MUNGU NI MWAMINIFU KWA KILA JAMBO
KWA WALE WANAOPENDA KUHUBIRI INJILI KWA JIA YA WIMBANI NA WANASHINDWA KUTUNGA NYIMBO TUWASILIANE ILI KUPEANA MBINU NYINGI ZA KUWEZA KUMSIFU MUNGU KWA ROHO NA KWELI  TAFADHALI WASILIANA NAMI KWA SIMU NO 0752407130 AU KWA BARUA PEPE emeldasakalani@gmail.com

HAKUNA KISICHO WEZEKANA KWA BWANA

  • mtegemee mungu katika kila bambo utafanikiwa je unamtegemea nani katika maisha yako?
     Mungu ni yule jana leo na hata milele ukimpa maisha yako kila utakacho hitaji kwake utapata je wahitaji nini kwa mungu//   usisite yeye ndiye muumba wa vyote anaweza kukusaidia
  • Weka tumaini kwa bwana